Mkuu wa Wilaya ya Magu, Mhe. Joshua Nassari leo ijumaa Novemba 22, 2024 ameongoza kikao cha kawaida cha baraza la biashara la Wilaya.
Akizungumza wakati wa kikao hicho kilichofanyika ofisini kwake DC Nassari ameutaka uongozi wa Halmashauri kushirikiana na wananchi kwaajili ya kupata na kutenga maeneno ya uwekezaji.
Aidha, amesisitiza ushirikiano kati ya serikali, sekta binafsi na wawekezaji ili kuinua na kukuza fursa za uchumi zinazopatikana Wilayani Magu kukuza uchumi wa Wilaya na taifa kwa ujumla.
Vilevile ameitaka idara ya ardhi kuratibu mpango wa upimaji ardhi shirikishi ili kutenga maeneo ya uwekezaji ili yaweze kupata wawekezaji kwenye sekta mbalimbali ikiwemo ya viwanda na kilimo.
Akizungumzia suala la stendi na soko la kisasa mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Magu, Mohamed Ramadhani amesema Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imetenga kiasi cha Shilingi Bilioni 4.6 kwaajili ya ujenzi soko la kisasa na bilioni 6.8 kwaajili ya ujenzi wa stendi ya Magu.
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Magu. Haki zote zimehifadhiwa