Mkuu wa Wilaya ya Magu Mheshimiwa Philemon Sengati (PhD) leo tarehe 14.03.2019 amezindua bodi ya maji Magu mjini itakayofanya kazi sanjali na Mamlaka ya Maji Magu Mjini. amewapongeza wajumbe wa Bodi mpya ya maji kwa uteuzi katika nafasi zao uliofanywa na Waziri katika Ofisi ya Rais –TAMISEMI Januari 31,2019. Na kwamba bodi hiyo itadumu kwa miaka mitatu,
Aidha Mheshimiwa DC ameitaka Bodi hiyo kufanya kazi kwa weledi, uadilifu na uaminifu wa hali ya juu ili kuleta matokeo chanya wakati Serikali inakamilisha ujenzi wa mradi mkubwa wa Maji ambao utaendeshwa na Mamlaka ya Maji Magu mjini chini ya Bodi hii mpya.
Awali Mkuu wa Idara ya Maji mhandisi James Kionaumela ametoa ufafanuzi kwa Wajumbe wa Bodi mpya Majukumu ya Mamlaka ya maji na majukumu ya Bodi ya Maji kwa ujumla pia amesema kuwa Bodi hii itasaidia Mamlaka katika kutatua kero za maji, kutoa elimu kwa jamii na kuwaleta pamoja watumiaji maji.
Naye Meneja wa Mamlaka ya maji Mhandisi Lubapula Mayombya ambaye pia ni katibu wa Bodi amesema kuwa wanakusudia kuchapa kazi kadri uwezo na ufahamu wao ili kuihudumia jamii kwa usawa, uwazi Pia ametoa wito kwa Wajumbe wa bodi kuishauri na kusimimamia Mamlaka ya maji kwa lengo la kufanya kazi wa pamoja kama timu. Vilevile amebainisha kuwa Bodi ina wajumbe saba na ina Mwenyekiti mwenye weledi na uzoefu mkubwa hasa kwa kuzingatia kuwa ni Hakimu mstaafu Mzee Issa Hozza.
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Magu. Haki zote zimehifadhiwa