Zoezi la usafi wa mazingira kwa wananchi wa Magu litakuwa ni endelevu ili kujikinga na kutokomeza magonjwa ya mlipuko, haya yamejili katika kikao cha wadau wa Usafi na uhifadhi wa mazingira kilichoitishwa na mkuu wa Wilaya ya Magu Dr. Philemon Sengati katika ukumbi wa mikutano ya halmashauri ya magu.
Mkutano huo wa wadau umewakutanisha Wafanyabishara, Wafugaji, Waendesha bodaboda,Wakuu wa idara wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji (W), Viongozi wa vyama vya siasa, Viongozi wa madhehebu ya dini na Wazee mashuhuri. Ambapo wameishauri serikali kuongeza jitihada katika zoezi la usimamizi, uratibu, udhihiti wa uchafuzi wa mazingira kwa kutumia mgambo wakishirikina na viongozi wa Vitongoji, Vijiji na kata.
DC Sengati amewataka watalaam wa afya wawaelekeze Mgambo namna ya kufanya katika suala zima la usafi wa mazingira, na taarifa dhidi ya waharibifu na wachafuzi wa mazingira zitolewe kwa viongozi wa Serikali za mitaa kwa hatua na utatuzi na ikishindikana Wahusika wafikishwe kwenye vyombo vya sheria ikiwa ni hatua mwisho kabisa.
Akizungumza na Wananchi wa Magu kupitia wadau wa usafi wa mazingira, DC Sengati ametoa wito kwa viongozi wote kuendesha kampeni ya usafi na uhifadhi wa mzingira katika mikutano yao ili kuwahamasisha wananchi kutunza mazingira kwa ajili afya zao, na kuifanya Magu kuwa sehemu safi na yenye kuvutia katika utunzaji wa mazingira. Pia ameowaomba viongozi kufanya kazi kwa kushirikiana na kuwasiliana zaidi ili kuweza kutimiza ndoto za kuipendezesha Magu kupitia kampeni ya "MAGU MPYA BILA UCHAFU INAWEZEKANA".
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Magu. Haki zote zimehifadhiwa