Mkuu wa Wilaya Magu Mheshimiwa Dkt.. Philemon Sengati ameongoza kikao cha kwanza cha mwaka cha kamati ya ushauri wa kodi Wilaya.Kikao hicho kimefanyika Ofisini kwa Mkuu wa Wilaya na kuhudhuriwa na Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo ambaye pia ni Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Wilaya Ndg: Lutengano G. Mwalwiba. Kamati ya hiyo imehudhuriwa pia na wajumbe wake akiwemo Mheshimiwa Kiswaga Mbunge, Afisa Mtendaji wa Mamlaka ya Mji mdogo Magu, Mkuu wa Polisi wilaya, Meneja Wilaya wa Mamlaka ya mapato (TRA) ambaye nikatibu wa kamati hiyo, Afisa biashara wilaya, Mwenyekiti wa TCCIA na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya..
DC Sengati amesisitiza kuwa zoezi la ugawaji wa Vitambulisho vya wafanyabishara wadogo, vilivyotolewa na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, tayari vimeshapelekwa kwawatendaji wa vijiji ambao wanaendelea na kuwaratibu walengwa na kuwapatia kwa mujibu wa maelekezo yalitolewa na Serikali. Vilevile DC Sengati ameagiza kwa Wananchi wote kuwa suala kulipa kodi ni lazima hivyo wajitokeze mapema kwenye Ofisi za Mamlaka ya Mapato ili waweze kulipa kodi kama sheria inavyowataka.
Dkt. Sengati kupitia kikao hicho amemtaka menejawa mapato kuhakikisha kuwa anashughulikia tatizo la upungufu wa wafanya kazi katika Ofisi yake ili kuondoa kero inayowakwamisha kuwafikia walipa kodi kutokana na kukosekana kwa Dereva wa gari la TRA, aidha amesisitiza kuwa katika kipindi hiki “Sisi na Halmashauri tuko tayari kuwapatia ushirikiano ilimsikwame” amesema Dkt.. Sengati.
Wajumbe wa Kamati wamesisitiza Mamlaka ya mapato kushirikiana na Ofisi ya biashara Wilaya ili kufanikisha kuwabaini walipa kodi wenye sifa ya kutumia mashine za kielekitronic (EFD) ili waweze kushauriwa kuzipata na kuanza kuzitumia mara moja ili kuinua ukusanyaji wa mapato katika wilaya. Kamati imeshauri pia Mamlaka ya mapato iendelee na juhudi zake za kutoa elimu kwa walipa kodi na ikibidi kuwatembelea katika maeneo yao ya biashara hasa katika miji ya biashara ya kisesa, Nyanguge, Kabila na Mahaha.
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Magu. Haki zote zimehifadhiwa