Mkuu wa wilaya ya Magu ambaye pia mwenyekiti wa Kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya Dr. Philemon Sengati (PhD), amewatembelea wafungwa na mahabusu 190 walioko katika gereza la Wilaya ya Magu, amepata wasaa wa kuwasiliza, kuongea nao pia amewapatia msaada wa mahitaji mbalimbali kwa ajili ya matumizi yao.
DC Sengati amewasili gerezani hapo akiwa ameongozana na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya, ambapo wafungwa na mahabusu wamemweleza matatizo mbalimbali yanayowakabili yakiwemo kesi zao kucheleweshwa na ukosefu wa maji ya kutosha.
Akijibu kero na Malalamiko DC Sengati amewataka Wafungwa na Mahabusu kuwa na imani na uvumilivu haya ambayo yanatoakana na Ucheleweshaji wa kesi kwa kigezo cha upelelezi OCD “nakuomba ulishughulikie hasa kwa makosa madogo madogo, na mengine yanayohusu mhimili wa Mahakama mawasiliano yatafanyika ili kutatua hizi kero zenu kwani tunaamini watazifanyia kazi” amesema Sengati. Suala la Maji amewataka wafungwa kuwa na subira kwani siku sio nyingi mradi mkubwa wa Maji Magu Mjini utazinduliwa.
Aidha DC amewapatia wafungwa mahitaji mbalimbali kama vile Sabuni, Mafuta ya kupakaa, Miswaki na Dawa ya meno.
Wafungwa na Mahabusu wamemshukuru DC Sengati na kusema kuwa “Asante Ndugu Mkuu wa Wilaya na msafara wako kwa kutukumbuka tumefarijika kuwa tuna kiongozi anayejua kuwa sisi ni wahitaji, Tunakuomba kila upatapo fursa njoo utusalimie na utusikilize na Mkuu wetu wa Gereza na Maofisa wote wa magereza wanatulea kwa maadili mema tunaamini tumeshabadilika. Tufikishie Salamu zetu kwa Mheshimiwa Rais kuwa tunampongeza sana kwa Kazi nzuri na kitendo chake cha kwenda Butimba Gerezani kuongea na Wafungwa na mahabusu kimetuaminisha kuwa sasa haki itatendeka"
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Magu. Haki zote zimehifadhiwa