Maofisa wa Maliasili katika Wilaya ya Magu Wamefanikiwa kuua Mnyama Hatari (Chui) aliyevamia nyumbani kwa Mkurugenzi Mtendaji (W). chui huyo ameruka Fensi na kuingia ndani na kupambana na Mbwa wawili wa MKurugenzi ambapo mbwa hao waliachiwa majeraha makubwa. Usiku uliofuata Chui huyo alirejea tena, ndipo walinzi wa Mkurugenzi na Maofisa Wanyama Pori wakafanya kazi ya ziada na kufanikiwa kumuua chui huyo.
Pongezi nyingi ziwafikie Maofisa wa kitengo cha Wanyama Pori kwa kazi nzuri waliyoifanya kwa kumuua mnyama huyo hatari ambaye angeweza kuhatarisha maisha ya wananchi katika Mji wa Magu.
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Magu. Haki zote zimehifadhiwa