Afisa Mipango na Takwimu kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji (W) amewasilisha mapitio ya Bajeti ya Mwaka 2016/2017, 2017/2018 na Rasimu Mpango wa bajeti ya mwaka 2018/2019 mbele ya wajumbe wa Baraza la Madiwani la Halmashauri. Ameeleza kwamba, katika kuandaa bajeti ya mwaka 2018/2019, Halmashauri imejikita katika miradi inayolenga kuleta matokeo chanya na yenye kugusa maisha ya wananchi moja kwa moja, kukamilisha viporo na madeni ya wazabuni kabla ya kuanzisha miradi mipya, na miradi inayolenga kuzingatia malengo endelevu 17 ya mwaka 2030 (SDGs).
Kwa kifupi ameeleza vipaumbele vya bajeti ya Halmashauri kuwa ni kama ifuatavyo;-
Wajumbe wa Baraza la Madiwani wakiongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri Mheshimiwa Hilali Nassoro Elisha ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Nyanguge, wamepongeza menejimenti kwa ushirikiano ulioonyeshwa katika kuandaa vikao vya bajeti kuanzia CMT, baraza la wafanyakazi, DCC, Kamati za kudumu za Halmashauri, hadi Baraza la Madiwani, pia wamepongeza mpango wa Bajeti kwani umezingatia masuala mtambuka kama vile ushirikishwaji wa Wananchi na wadau wa masuala ya jinsia , mazingira, vijana, UKIMWI, na kuzuia Rushwa.
Aidha baada ya pongezi hizo, wajumbe kwa kauli moja wamepitisha rasimu ya Mpango wa bajeti ya mwaka 2018/2019 ambapo Halmashauri ya Wilaya ya Magu imeomba kuidhinishiwa Jumla ya Tshs.45,057,115,000.00 kutoka vyanzo vyake mbalimbali na kutoka ruzuku ya serikali kuu.
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Magu. Haki zote zimehifadhiwa