Baraza la Madiwani limejadili rasimu ya mpango wa bajeti katika mkutano Maalum uliofanyika katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Magu chini ya Mwenyekiti wa Halmashauri.
Akiwasilisha rasimu hiyo ya Bajeti Mkurugenzi Mtendaji (W) ametaja baadhi ya mambo muhimu yaliyozingatiwa katika bajeti ya 2020/21 ambayo ni kujikita katika miradi inayolenga kuleta matokeo chanya yenye kugusa maisha ya wananchi moja kwa moja, kukamilisha miradi viporo, miradi ya malengo endelevu 17 ya mwaka 2030 (SDGs), ushirikishwaji wa wananchi, kutekeleza mpango wa ugatuaji wa madaraka na rasilimali fedha (D by D), O &OD iliyoboreshwa kwa kuzingatia jitihada za jamii, mpango wa lishe kitaifa kutenga asilimia 10 ya mapato ya ndani kwa ajili ya mifuko ya maendeleo ya wanawake vijana na walemavu, na kuimarisha ukusanyaji wa Mapato ya Halmashauri.
Aidha ametaja vipaumbele vya bajeti vya Halmashauri kwa Mwaka 2020/21 ambavyo ni kuanzisha miradi ya kimkakati, ukamilishaji wa vyumba vya madarasa 10 na nyumba za walimu 5, kukamilisha ujenzi wa zahanati 9 na kupunguza uhaba wa watumishi kwa kuajiri watumish wapya 764 wa kada mbalimbali.
Kupitia mjadala wa wajumbe wa baraza la Madiwani wameridhia kupitisha bajeti jumla ya Tshs. 49,231,177,221.00 kutoka vyanzo mbalimbali vya Halmashauri na kutoka Ruzuku ya serikali kuu kwa mwaka wa fedha 2020/21.
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Magu. Haki zote zimehifadhiwa