Katibu Mkuu wa Wizara ya maji Prof. Jamal Katundu ameupongeza uongozi na safu nzima ya Watendaji wa Wilaya ya Magu kwa usimamizi mzuri na utekelezaji wa mradi wa kuhimili mabadiliko ya tabia ya nchi katika bonde la ziwa victoria ( adapting to climate change in lake victoria basin - ACC- LVB) kupitia kamisheni ya Bonde la Ziwa victoria ( LVBC) unaotekelezwa Wilaya ya Magu.
Pro Katundu ameyasema hayo akiwa ziarani katika kijiji cha Nghaya Wilayani Magu ambapo alitembelea na kukagua mradi unaotekelezwa na LBVC ikiwemo kisima cha Busalanga kinachopeleka maji katika shule ya msingi Nghaya , shughuli za uvunaji wa maji ya mvua, bustani ya mbogamboga na shughuli za uoteshaji wa miche na upandaji miti ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo Prof. Katundu amesema mradi huo ukifanyika kwa ufanisi utakua na matokeo chanya kwa wananchi kwani watajipatia kipato sambamba na kutunza mazingira kwasababu mradi huu ni kichocheo cha utunzaji wa mazingira na kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi.
" tumeoa huu mradi mkubwa amabao umeanzishwa hapa lengo kubwa ikiwa ni kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi na mradi unaendelea vizuri na matokeo yake yanaonekana hivyo muhimu ni kuona namna ya kufanya upanuzi wa mradi huu ili uendelee kuleta matokeo chanya kwa wananchi.
Utekelezaji wa Mradi huu wa kuhimili mabadiliko ya Tabianchi katika kijiji cha Ng’haya unalenga kupunguza athari za mabadiliko ya tabianchi kwa jamii inayoishi katika bonde la Ziwa Victoria kwa nchi za Burundi, Kenya, Rwanda, Tanzania na Uganda.
Vilevile kujenga uwezo wa jamii inayoishi katika maeneo hayo kuweza kuhimili mabadiliko ya Tabianchi kwa kutumia teknolojia za uvunaji wa maji ya mvua, maji chini ya ardhi, kilimo kinachohimili mabadiliko ya Tabianchi, mbinu zinazozingatia mifumo ya ikolojia katika shughuli zao za kijamii na kiuchumi.
Shughuli zingine zinazotekelezwa Wilayani Magu kupitia mradi huo kwa lengo la kuongeza kipato kwa jamii kupitia kilimo cha kisasa cha bustani na mboga mboga (kupitia vitalu nyumba) vikundi.
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Magu. Haki zote zimehifadhiwa