Mkuu wa wilaya ya magu Mh Rachel kassanda ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa wilaya hiyyo siku ya tarehe 20/02 alifanya ziara ya kutembelea miradi minne inayotekelezwa wilayani humo kupitia mfuko wa kunusuru kaya masikini TASAF ambayo (ZAHANATI katika kijiji cha bugando,nyumba ya watumishi zahanati ya ihayabuyaga,nyumba ya watumishi shule ya masingi lutale pamoja na vyumba viwili vya madarasa shule mpya ya sekondari Igekemaja ) mh mkuu wa wilaya pamoja na kamati waliridhishwa na usimamizi mzuri wa fedha kwa kwa watendaji wote waliosimamia miradi yote nakuwaomba wakamillishe haraka sehemu ndogondogo zilizobaki ili niradi hiyo ianze kutoa huduma haraka kwa wananchi aidha mkuu wa wilaya hiyo alipata nafasi ya kuzungumza na wananchi wa maeneo hayo na kuwaomba waitunze miradi hiyo ambayo imetekelezwa na fedha za serikali lakini pia na mchango wa nguvu za wananchi wenyewe aidha mh RACHEL KASSANDA akiongea na waandishi wa Habari kwa niaba ya wananchi wa wilaya ya magu alimshukur mh rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania dk samia suluhu hassan kwa kuendelea kutoa fdha nyingi zinazotekeleza miradi mbalimbali katika wilaya ya magu naye pia kuahidi kuendelea kusimamia matumizi ya fedha hizo wakati wote wa utekelezaji wa miradi itayoletwa na serikali wilayani magu
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Magu. Haki zote zimehifadhiwa