Kamati ya fedha, uongozi na mipango ya Halmashauri ya Wilaya ya Magu ikiongozwa na Mwenyekiti wake Mh. Simon Mpandalume imefanya ziara ya kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika kipindi cha robo tatu ( Januari-Machi , 2024) tarehe 29/04/2024 .
Miradi iliyotembelewa ni pamoja na uendelezaji wa shule mpya ya sekondari Sayaka , ujenzi wa zahanati mpya ya kijiji cha kinango, ujenzi wa ofisi ya mtendaji kijiji cha kinango.
Miradi mingine ni ujenzi wa madarasa mawili na ofisi moja katika shule ya msingi Mwamanyili na ukamilishaji wa vyumba viwili vya madarasa na ofisi moja shule ya msingi Mwahuli Kata ya Bukandwe.
Aidha Kamati ilikagua athari za matundu ya vyoo yaliyobomoka kutokana na athari za mvua zinazoendelea kunyesha katika shule ya sekondari shishani na shule ya msingi Busekwa .
Akizungumza wakati wa ziara hiyo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Magu Mhe Simon Mpandalume amewapongeza wananchi kwa nguvu kazi ya kuanzisha miradi mbalimbali na ya maendeleo huku akiahidi kua Halmashauri itapeleka fedha za mapato ya ndani kwaajili ya kukamilisha miradi hiyo.
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Magu. Haki zote zimehifadhiwa