Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Magu Mh. Simon Mpandalume amesema zao la pamba ambalo linalimwa kwa wingi Wilayani Magu lina mchango mkubwa katika kukuza mapato ya halmashauri kutokana na makusanyo yanayopatikana msimu wa mavuno na mauzo ya zao hilo.
Mh. Mpandalume ameyasema hayo wakati akifungua mkutano wa baraza la madiwani kwaajili ya kupitia taarifa za utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa kipindi cha robo ya kwanza uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri Januari 24, 2025.
Amesema ni muhimu bodi ya pamba, vyama vya ushirika , wataalamu wa kilimo wa halmashauri kushirikiana na wawekezaji na wakulima wa zao la pamba ili kuongeza tija ya uzalishaji wa zao hilo.
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Magu. Haki zote zimehifadhiwa