Imeelezwa kuwa kukamilika kwa Zahanati ya kijiji cha Kinango kilichopo Kata ya Nyigogo Wilayani Magu itasaidia kupunguza changamoto ya wanachi wa kijiji hicho kutembea umbali mrefu kufata huduma ya afya katika jirani cha Ychobela.
Hayo yameelezwa na mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Magu Simon Mpandalume (Diwani Kata ya Nyigogo) wakati akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kinango katika mkutano wa hadhara.
Akizungumza na wananchi hao Mpandalume amesema kuwa Halmashauri imeshapeleka fedha ya mapato ya ndani kwaajili ya kukamilisha ujenzi wa jengo la zahanati hiyo.
Katika hatua nyingine Mpandalume amesema serikali imetenga fedha za mapato ya mapato ya ndani kwaajili ya kukamilisha ofisi ya mtendaji wa kijiji cha Kinango.
Kuhusu huduma ya umeme Mpandalume amesema katika vijiji 82 vya Wilaya ya Magu, vijiji 81 vina umeme isipokuwa kijiji kimoja tu cha Ijinga ambacho kipo kisiwani na tayari serikali imekiweka katika mpango wa kukipelekea umeme na katika vijiji vingine kazi iliyobaki ni kupeleka umeme katika vitongoji.
Amesema katika bajeti ya mwaka wa fedha 2025-2026 baraza limeweka baadhi ya vitongoji vya kijiji cha Kinango kwaajili ya kupelekewa huduma ya umeme.
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Magu. Haki zote zimehifadhiwa