Wafanyabiashara wa eneo la kibiashara Ilungu lililopo kata ya Nyigogo wilayani Magu mkoani Mwanza leo Ijumaa wameshiriki zoezi la usafi wa mazingira kwa kusafisha mitaro ya barabara ya Ilungu-Kinango ili kuunga mkono jitihada za halmashauri ya Wilaya ya Magu katika jitihaza za kusahamasisha usafi wa mazingira.
Kwa mujibu wa Mkuu wa Kitengo cha usimamizi wa taka ngumu na usafi, Francisco Ndazi, zoezi hilo ni endelevu katika maeneo mbalimbali ya halmashauri hiyo.