Viongozi wa dini Wilayani Magu wamehimizwa kuendelea kuiombea nchi ya Tanzania iendelee kuwa na amani pamoja na kumuombea Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ili aendelee kufanya kazi na kuwatelea watanzania maendeleo .
Wito huo umetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Magu Mh. Rachel Kassanda wakati wa kikao na viongozi wa dini pamoja na viongozi wa kimila kilichofanyika leo Ijumaa Desemba 29, 2023 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Magu.
Akizungumza katika kikao hicho kilichowakutanisha vionozi wa dini na viongozi wa kimila wakiwemo Machifu DC Kassanda amesema kuwa viongozi wa dini ni wadau muhimu katika jamii hivyo ni vyema wakatumia mafasi zao katika kuendelea kuzungumzia umuhimu wa amani wnapokuwa katika nyumba zao za ibada.
"Niwaombe viongozi wa dini wachungaji, maaskofu, masheikh, machifu na wengine wote kuendelea kumuombea Rais Samia kwani maombi yenu ni muhimu sana katika kumpa nguvu na maarifa ya kuliongoza taifa letu " amesema.
Aidha DC Kassanda amewataka viongozi hao kuhubiri amani na utulivu kwa waumini wao haswa kuelekea sikukuu ya mwaka mpya ili kukemea vitendo vyote vya uvunjifu wa amani vinavyoweza kujitokeza kipindi cha sikukuu ili wananchi wafurahie sikukuu kwa amani na utulivu.
Akitoa salamu za Rais Samia kwa viongozi hao DC Kassanda amemshukuru Mh. Rais kwa kuendelea kupeleka fedha nyingi kwaajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo katika Wilaya hiyo ikiwemo ujenzi wa shule mpya , zahanati na barabara ambazo zimekua chachu ya maendeleo katika Wilaya ya Magu.
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Magu. Haki zote zimehifadhiwa