Katika doria zinazoendelea katika ziwa Victoria, Halmashauri ya Wilaya ya Magu kupitia Kitengo cha Uvuvi imekamata samaki wadogo ambao waliokuwa wanasafirishwa kinyemela katika mifuko na ndoo za plastic. Kitengo hicho cha uvuvi kimeendelea kutekeleza majukumu ya kuhakikisha rasilimali za uvuvi katika ziwa Victoria zinalindwa kwa kudhibiti utumiaji wa zana zauvuvi zilizopigwa marufuku.
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Magu. Haki zote zimehifadhiwa