Pongezi hizo zimetolewa na Waheshimiwa Madiwani katika Mkutano wa kawaida wa baraza la madiwani uliofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Magu. Mkurugenzi Mtendaji (W) amewasilisha shule hizo mbele ya wajumbe wa baraza la Madiwani ambapo amesema kuwa Shule ya Sekondari Magu imekuwa ya 4 kati ya Shule 25 za mkoa wa mwanza na Shule ya Sekondari Lugeye imeshika nafasi ya 14 kati ya shule 25 za Mkoa wa Mwanza.
Shule hizo zimewakilishwa na wakuu wa shule na walimu wa taaluma, Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Hilali N. Elisha amemkaribisha Mbunge wa jimbo la Magu Mhe Destery B. Kiswaga kukabidhi vyeti vya pongezi kwa walimu hao ambao shule wanazosimamia zimefanya vizuri kwenye mtihani wa kidato cha sita mwaka, 2017.
Aidha baada ya walimu hao kukabidhiwa vyeti, Mwenyekiti wa Halmashauri amewapongeza kwa juhudi walizofanya hadi shule zimefanya vizuri, pia amepongeza wadau wote walioshiriki katika kuimarisha taaluma na kuongeza kiwango cha ufaulu katika shule hizo na kusisitiza kuendelea kusimamia vizuri Elimu ili shule zote katika Wilaya ya magu zifanye vizuri zaidi kwenye Matokeo ya Mtihani wa Mwisho.
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Magu. Haki zote zimehifadhiwa