Hayo yamejiri katika ziara ya Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Dr. Mary Machuche Mwanjelwa iliyofanyika tarehe 03.10.2019 wilayani Magu. Naibu Waziri ameambatana na Baadhi ya Makamishna wa Tume ya Utumishi wa Umma walioteuliwa na Mheshimiwa Rais, Lengo la ziara likiwa ni kusikiliza na kutolea ufafanuzi changamoto zinazowakabili watumishi wa Umma .
Amesema Serikali ya awamu ya tano inawajali, inawapenda na inawathamini watumishi wa Umma na kuwa mtumishi wa Umma ni Fursa na wanahudumia wananchi katika maeneo yao. “kila Mtumishi anatakiwa kupenda na kujali kazi yake kwa nafasi yake aliyonayo, awajibike ipasavyo na kuacha kufanya kazi kwa mazoea katika serikali hii ya awamu ya tano. Waajiri wote Watenge Muda na siku kwa ajili ya kukutana na watumishi wa Umma na kusikiliza kero zao na kuzitatua kwa wakati” amesema Naibu Waziri.
Pia amewataka Watumishi wa Umma kuzingatia Sheria, Taratibu, Kanuni na Miongozo inayotolewa na serikali na kufanya kazi kwa bidii, weledi, umahiri, uzalendo na ubunifu mkubwa katika maeneo ya kazi na kuzingatia OPRAS kwa vitendo na sio nadharia. “Waajiri watende haki kwa watumishi pindi wanapokuwa na changamoto na kutoa huduma bora kwa wananchi. Suala la Mahusiano kazini ni muhimu sana kwa watumishi waliopewa dhamana ya kuongoza Taasisi. Aidha Barua yoyote inayokwenda nje ya Taasisi lazima ipite kwanza kwa mwajiri wa Taasisi husika”.
Awali Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya Dr. Philemon Sengati amemshukuru sana Naibu waziri kwa kufika kuzungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Magu na amemhakikishia umoja, Mshikamano na uadilifu uliopo Magu wa kwendana na kasi ya Serikali ya awamu ya tano ya Dkt John Pombe Magufuli. Aidha ameeleza changamoto ya upungufu wa Watumishi katika wilaya ya Magu katika kada mbalimbali.
Nae Mbunge wa Jimbo la Magu Mheshimiwa Destery B. Kiswaga ameshukuru na kupongeza ujio wa Naibu waziri amesema “ katika ziara nilizofanya nimekutana na watumishi wote wa Umma katika tarafa zao wanazofanyia kazi wamenieleza changamoto zao ambapo nyigine zimepatiwa ufumbuzi na nyigine ambazo hazikuweza kupata ufumbuzi nilikuletea na umeshaanza kuzifanyia kazi” amesema Kiswaga.
Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Umma Ndugu John Michael Haule (Balozi) ameeleza kazi mbalimbali zinzofanywa na tume pamoja na watumishi wanaohudumiwa na tume hiyo yenye Makamishina 7 ambapo amesisitiza waajiri kutoa ushirikiano mkubwa katika tume hiyo. Aidha Sekretarieti ya tume hiyo imewasilisha mada ya Misingi ya sheria katika kusimamia haki na wajibu wa watumishi wa Umma.
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Magu. Haki zote zimehifadhiwa