Mratibu wa TASAF Magu Ndg. Daniel Sanyenge amepata Pongezi hizo Katika Mkutano Maalumu wa Baraza la Madiwani wa kupitia hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Uliofanyika Tarehe 20.08.2018 katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Magu. Aidha Mwenyekiti wa Baraza hilo amesema lengo la Halmashauri ni kuendelea kupata hati safi na kuepuka hoja za ukaguzi, hivyo ameagiza Mratibu wa TASAF Kuandikiwa hati ya pongezi kwa kazi nzuri aliyoifanya ya kufuta hoja.
Bi. Christina Bigambo (AAS) ameshauri wataalam wa Halmashauri wafanye juhudi ili hoja zifungwe na wajumbe wa kamati ya fedha kila mwezi wawe wanapewa taarifa ya idadi ya hoja zilizifungwa kila mwezi. Pia ameshauri kwa miradi ambayo fedha yake haifiki kwa Mwaka husika wa fedha, iwe inapangiwa tena bajeti kwa mwaka unaofuata ili kuepuka hoja za ukaguzi. Naye Mkurugenzi Mtendaji (W) amesema kwamba, mpango mkakati uliopo Kwa Halmashauri ya Magu ni Kuzuia hoja za ukaguzi.
Mkuu wa wilaya ameahidi kusimamia suala ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri, ambapo amewataka wataalam kubuni vyanzo vya mapato kwani “tunapaswa kuanza kujitegemea katika makusanyo ya mapato ya ndani kutoka vyanzo mbalimbali vya Halmashauri, lengo ni kuifanya Magu kuwa kinara katika ukusanyaji wa mapato ya ndani na kuondoa hoja zote zinazohusiana na mapato ya ndani”.
Wajumbe wa baraza hilo wametoa michango mbalimbali na kutoa maoni katika hoja za CAG ambapo lengo ni kufunga na kufuta hoja za ukaguzi katika Halmashauri ya Wilaya ya Magu.
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Magu. Haki zote zimehifadhiwa