Ushauri huo umetolewa katika Mkutano maalum wa Baraza la Madiwani wa kujadili hoja Za CAG kwa kipindi cha Mwaka wa Fedha, 2015/2016 uliofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Magu tarehe 11.08.2017. Wajumbe wa Baraza hilo wameshauri Menejimenti kufuata taratibu, kanuni sheria na Miongozo mbalimbali inayotolewa na Serikalia kwani kwa kufanya hivyo hoja zitapungua. Aidha wamesisitiza Vielelezo vyote vinavyohitajika kwa wakaguzi wa nje vitafutwe na kupelekwa kwa ajili ya uhakiki ili hoja zifungwe.
Wajumbe hao wameiomba Serikali kuleta fedha za Miradi ya Maendeleo kwa wakati ili miradi iweze kutekelezwa kwani hoja nyingi zimejitokeza kipindi cha nyuma kwa sababu za ukosefu wa fedha za miradi ya Maendeleo.
Katiba Tawala Mkoa wa Mwanza (RAS) amesisitiza menejimenti kutoa majibu mazuri kutokana na yanayokuwa yanahojiwa na Wakaguzi wa nje ili hoja za Ukaguzi zifutwe kwa wakati. Amepongeza Halmashauri ya Wilaya kwa kupata Hati Safi kwa Mwaka 2015/2016 ambapo amesema mikakati mizuri iwekwe ili Halmashauri iendelee kupata hati safi ambayo ni endelevu.
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Magu. Haki zote zimehifadhiwa