Mbunge wa Jimbo la Magu Mhe. Destery B. Kiswaga amekabidhi gari la kubebea wagonjwa katika kituo cha afya Kabila. Makabidhiano hayo yamefanyika tarehe 13.04.2018 ambapo ameelekeza gari hilo litumike kwa manufaa yaliyokusudiwa kwa kuzingatia maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli. amesisitiza wananchi wafanye kazi kwa bidii ili wajiletee maendeleo na watunze chakula vizuri kwa ajili ya kukabiliana na njaa katika maeneo yao.
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Magu. Haki zote zimehifadhiwa