Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayesimamia masuala ya Afrika Mashariki Mhe. Stephen Byabato (Mb.) ameupongeza Uongozi na safu nzima ya Watendaji wa Wilaya ya Magu kwa usimamizi mzuri wa utekelezaji wa wa Mradi wa Kuhimili Mabadiliko ya Tabia Nchi katika Bonde la Ziwa Victoria (Adapting to Climate change in Lake Victoria Basin – ACC – LVB) kupitia Kamisheni ya Bonde la Ziwa Victoria (LVBC) unaotekelezwa Wilaya ya Magu.
Naibu Waziri Byabato ameeleza hayo alipokuwa ziarani katika Kijiji cha Ng’haya Wilayani Magu ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kikazi katika Kanda ya Ziwa ambapo anatembelea na kuona ufanisi wa miradi mbalimbali ya Jumuiya ya Afrika Mashariki inayotekelezwa kupitia LVBC.
Akipokea taarifa ya utelekezaji wa mradi huo uliogharimu kiasi cha Shilingi 656,785,965 iliyowasilishwa na Watendaji wa Wilaya ya Magu ambapo pia alipata nafasi ya kutembelea miradi hiyo ameleza namna alivyofarijika kuona mradi huo ulivyochangia ustawi wa kiuchumi kwa wananchi wa kijiji cha Ng’haya.
“Nimefarijika sana na namna mradi huu ulivyowanufaisha wananchi kwa kuwaongezea kipato kupitia miradi iliyotajwa kwenye taarifa yenu ambayo pia muda mfupi ujao nitaenda kuitembelea. Natoa pongezi sana kwa Uongozi na safu nzima ya Watendaji wa Wilaya kwa namna mlivyosimamia utekelezaji wa mradi huu na kufikia malengo mliyojiwekea” Alieleza Naibu Waziri Mhe.Byabato
Utekelezaji wa Mradi huu wa kuhimili mabadiliko ya Tabianchi katika kijiji cha Ng’haya unalenga kupunguza athari za mabadiliko ya tabianchi kwa jamii inayoishi katika bonde la Ziwa Victoria kwa nchi za Burundi, Kenya, Rwanda, Tanzania na Uganda. Vilevile kujenga uwezo wa jamii inayoishi katika maeneo hayo kuweza kuhimili mabadiliko ya Tabianchi kwa kutumia teknolojia za uvunaji wa maji ya mvua, maji chini ya ardhi, kilimo kinachohimili mabadiliko ya Tabianchi, mbinu zinazozingatia mifumo ya ikolojia katika shughuli zao za kijamii na kiuchumi.
Shughuli zingine zinazotekelezwa Wilayani Magu kupitia mradi huo kwa lengo la kuongeza kipato kwa jamii kupitia kilimo cha kisasa cha bustani na mboga mboga (kupitia vitalu nyumba) vikundi
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Magu. Haki zote zimehifadhiwa