Mkuu wa mkoa wa Mwanza mhandisi Robert Gabriel leo tar 21/04/2022 amepokea miradi mitano ya AFYA yenye thamani ya zaidi ya millioni 950 fedha ilitolewa na serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania katika kuboresha huduma za afya wilayani magu miradi hiyo inahusisha jengo pacha litakalotoa huduma za uzazi na upasuaji,maabara na nyumba ya mtumishi kituo cha afya kisesa, zahanati ya kata ya Matale, jengo la x-ray zahanati ya Kahangara,jengo la maabara hospitali ya wialaya ya magu pamoja na jengo la wagonjwa wa nje kituo cha afya Shishani .
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Magu. Haki zote zimehifadhiwa