Katibu tawala wa Wilaya ya Magu Jubilate win Lawuo amewaongoza watumishi wa Wilaya ya Magu kwenye maombi na dua ya kuliombea Taifa katika kipindi hiki cha kuelekea maadhimisho ya miaka 60 ya muungano.
Watumishi mbalimbali wa Halmashauri na taasisi zilizopo Wilaya ya Magu na viongozi wa dini wamejitokeza kushiriki katika maombi hayo.
Akizungumza wakati wa maombi hayo DAS Lawuo amewataka viongozi wa dini na watanzania kuendelea kuiombea nchi kua na amani na utulivu kwa manufaa ya Taifa.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Magu Mohamed Ramadhan Kyande amewataka watanzania kuendelea kuenzi, kuthamini na kudumisha Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ili kuendeleza Amani na kupata maendeleo.
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Magu. Haki zote zimehifadhiwa