Halmashauri ya Wilaya ya Magu imesema kuwa katika mwaka wa fedha 2023-2024 imejipanga kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo iliyoanzishwa na wananchi kwa kutumia mapato ya ndani na fedha za serikali kuu ili kukidhi matarajio ya wananchi wa Wilaya ya Magu kupata maendeleo na kutatua changamoto mbalimbali.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Magu Mpandalume Simon wakati wa kikao cha Baraza la madiwani kupitia hesabu za mwisho wa Mwaka 2022/2023 kilichofanyika katika ukumbi wa CCM Wilaya ya Magu ambapo alibainisha kuwa uongozi wa Halmashuri hiyo una jukumu la kufanya kazi kwa bidii na ushirikiano ili kufikia malengo hayo na kukidhi matarajio na kiu ya wananchi kupata maendeleo katika maeneo yao.
" Tunayo miradi mingi ambayo wananchi wameanzisha ikiwemo maboma mbalimbali ya madarasa , zahanati na nyumba za watumishi hivyo kama Halmashauri tunalo jukumu la kuhakikisha kwamba tunakusanya fedha nyingi kupitia mapato ya ndani na kumuomba Rais kuleta fedha za miradi ili tuweze kukamilisha miradi hiyomm amesema Mpndalume"
Aidha Mpandalume amehimiza ushirikiano kwa watumishi na viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Magu ili kufanya kazi kwa bidii na kufikia malengo ya kukusanya mapato ya ndani kwa kiwango kikubwa na kutelekeleza miradi ya maendelo katika Wilaya hiyo.
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Bukandwe Michael Mathias amesema katika Mwaka wa Fedha 2023-2024 Halmashauri imejiwekea malengo ya kukusanya mapato zaidi ya sh Bilioni 4 na kubainisha kuwa wamejipanga kuhakikisha fedha hizo zinakusanywa na kuvuka lengo kwa kukusanya vizuri na kudhibiti mianya yote inayosababisha upotevu wa mapato.
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Magu. Haki zote zimehifadhiwa