“Mungu ushukuriwe kwa mema mengi hasa Neema ya kuishi, Afya na Baraka nyingi anazotukirimu. Leo tarehe1.8.2020 hadi 8.8.2020 maadhimisho ya Nane nane yalifanyika katika Viwanja vya Nyamhongolo Kanda ya Ziwa Magharibi, maonesho hayo yalishirikisha Mashirika, Taasisi, Asasi, Makundi ya Wajasiriamali na wadau wengine wa Kilimo katika kusherehekea siku hii Adhimu ya Wakulima. Halmashauri yetu ya Magu ni miongoni mwa Halmashauri 22 zilizoshiriki maadhimisho hayo na kuibuka kidedea katika Kundi la Halmashauri, Hongereni sana wana Magu wote” amesema DED Magu DC Bw. Lutengano George Mwalwiba.
“Nawapongeza Watumishi wote wa Halmashauri kwa maandalizi mazuri, jitihada na weledi wa hali ya juu katika kusababisha hili kutokea. Nawashukuru Wakuu wa Idara ya Kilimo na Mifugo pamoja na timu nzima ya maandalizi na Usimamizi wa Nanenane. Watumishi wote kwa ada yetu ya ushirikiano wa siku zote, sote ni timu moja. Namshukuru Mkuu wa Wilaya Bw Kalli pamoja na Kamati yote ya Usalama, RS kwa Ushauri na Uratibu kwani Magu ikifanya vizuri ni Mwanza ni Nchi yetu. Hivyo pia nimshukuru sana na kumpongeza Mh RC Mwanza, Mhe. John VK Mongella. Wadau wote wa Wilaya yetu na Wana Magu wote kwa Ujumla, hongereni na ahsanteni sana”. amesema DED Magu DC Bw. Lutengano George Mwalwiba.
“Hii inathibitisha dhamira yetu ya kuacha maneno na kufanya kazi , dhamira si kuwa wa kwanza bali ni kufanya kila jambo kwa ufanisi, ubunifu na nidhamu ili kutoa Huduma stahiki kwa Umma tunaoutumikia. Kilimo kinaajiri 70% ya Watanzania wote na Wataalam wanasema karibu 80% ya malighafi nyingi za Viwanda ni zao la Kilimo. Hivyo basi Halmashauri yetu inatoa ushindi huu kama mchango na jitihada katika kuifikia Tanzania ya Viwanda unaosimamiwa kwa umadhubuti mkubwa na Serikali ya awamu ya Tano” amesema DED Magu DC Bw. Lutengano George Mwalwiba.
Picha ya pamoja DED Magu na Wataalam wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi.
Picha ya pamoja DED magu, Wakuu wa idara, na wataalam wa kilimo na mifugo.
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Magu. Haki zote zimehifadhiwa