Maafisa usafirishaji Halmashauri ya Wilaya ya Magu wameshiriki kongamano la maafisa usafirishaji wa Serikali mkoani Mwanza uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mwanza.
Kongamano hilo lilifunguliwa na mkuu wa mkoa wa Mwanza Mh. Said Mtanda ambaye aliwataka maafisa hao wa usafirishaji kuendelea kujitambua , kutimiza wajibu wao na kufuata sheria za usalama barabarani.
Pia alitoa wito kwa baadhi ya viongozi wenye tabia ya kuwanyanyasa madereva kama vile kuwatumia muda mwingi pasipo sababu , kuingilia posho za mafuta waache tabia hiyo kwani haina tija na inajenga chuki.
Vilevile RC Mtanda alikabidhi vyeti vya pongezi kutokana na ushirikiano mzuri unaotolewa na maafisa usafirishaji Halmashauri ya Wilaya ya Magu.
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Magu. Haki zote zimehifadhiwa