Wazazi na walezi Wilaya ya Magu wametakiwa kuzingatia lishe bora kwa watoto wao ili kuboresha ustawi wao pamoja na ukuaji na kuepuka tatizo la udumavu.
Wito huo umetolewa na Mtendaji wa Kata ya Bujora Wilayani Magu Bi. Salome Bulugu wakati wa maadhimisho ya siku ya afya na lishe kata ya Bujora robo ya tatu 2024.
Akizungumza wakati wa maadhimisho hayo Bi Salome amewahimiza wananchi kuzingatia lishe bora kwani lishe kula sio kujaza tumbo bali kuzingatia ulaji bora wa chakula.
Aidha aliwakumbusha wananchi kuwa Agenda ya Lishe ni kipaumbele katika jamii maana lishe bora ni msingi imara wa maendeleo katika ujenzi wa Taifa lenye tija.
" lishe bora husaidia kupambana na utapiamlo na udumavu kwa watoto hivyo wazazi tuungane kwa pamoja kuhakikisha tunasimamia lishe bora kwa watoto" .
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Magu. Haki zote zimehifadhiwa