Kamati ya ulinzi na usalama Halmashauri ya Wilaya ya Magu ikiongozwa na mkuu wa wilaya Mhe. Joshua Nassari imefanya ziara ya kukagua utoaji wa huduma katika hospitali ya Wilaya ya Magu, kukagua majengo mapya ya wodi ya mama na mtoto, wodi ya wanaume na stoo ya dawa.
Aidha, kamati hiyo ilikagua mfumo wa kukusanya mapato ya Hospitali ya Wilaya ya Magu ( GOT- HOMIS ) na kueleza kuridhishwa na mwenendo wa ukusanyaji wa mfumo huo ambao umesaidia kuongeza mapato ya hospitali kwa zaidi ya asilimia 100.
Wakati wa ziara hiyo mkuu wa Wilaya ya Magu Mhe. Joshua Nassari alizungumza na wananchi ambao walifika hospitalini hapo kupata huduma za afya ambao walipongeza ubora wa huduma unaotolewa hospitalini hapo
Akizungumza baada ya kukagua utoaji wa huduma hospitalini hapo DC Nassari amewapongeza watoa huduma za afya na kuwasisitiza kuendelea kufanya kazi kwa bidii na kuzingatia misingi ya utumishi katika kutoa huduma.
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Magu. Haki zote zimehifadhiwa