Bonanza hilo la Miaka 54 ya Muungano limefunguliwa na Mgeni rasmi Mheshimiwa Khadija Nyembo ambae pia ni Mkuu wa Wilaya ya Magu. Maadhimisho hayo yamefanyika leo tarehe 26.04.2018 katika viwanja vya Magu Sekondari ambapo watumishi kutoka Halmashauri za Bunda, Misungwi, Ilemela, Kwimba na Magu wameshiriki katika Bonanza hilo. Kabla ya Kuanza Bonanza hilo watumishi wa Halmashauri ya wilaya Magu Wameshirikiana kufanya Usafi Katika Hospitali ya Wilaya.
Aidha watumishi wameshiriki vizuri Katika michezo mbalimbali ikiwemo riadha, Mpira wa mguu, Mpira wa wavu, mpira wa mkono na mpira wa pete. Pia wamejiotolea kupima afya zao na kutoa damu katika maadhimisho hayo.
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Magu. Haki zote zimehifadhiwa