Mkuu wa Wilaya ya Magu Mheshimiwa Philemon Sengati (PhD) ameongoza Baraza la biashara la Wilaya ya Magu katika ukumbi wa Mikutano wa Halmshauri ya Wilaya ya Magu kwa mara ya kwanza tangu Wilaya hiyo kuanzishwa mwaka 1974. Ameunda baraza hilo mwezi February 2018, likihusisha Wajumbe 20 kutoka sekta binafsi na wengine 20 wakitokea sekta ya Umma.
Mkuu wa Wilaya ya Magu kwa mujibu wa mwongozo wa baraza la Biashara ndiye Mwenyekiti wa Baraza, ambaye wakati akilihutubia baraza wakati wa ufunguzi amesema kuwa anapenda kuona baraza hilo likiwa na matokeo chanya na kwamba yeye yuko tayari kushirikiana na wajumbe pamoja na wadau wa kada mbalimbali ili kuboresha mazingira ya uwekezaji na biashara kwa ujumla. Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya Fundikira Said yeye ametoa ufafanuzi wajibu na nafasi ya baraza kuwa ni kuimarisha ushirikiano kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi katika kushauriana ili kuondoa vikwanzo na kutatua changamoto ili kuwezesha kuwa na maendeleo endelevu.
Afisa Biashara wa Wilaya ya Magu Bi Sarah Budimu ametoa ufafanuzi wa fursa zilizopo katika Wilaya ya Magu ikiwemo ardhi yenye rutuba, Ziwa Victoria, Miundo mbinu bora ya barabara, Wajumbe wa baraza hasa waliotoka sekta binafsi wamempongeza DR. Sengati (PhD) kwa uchapa kazi wake ni katika kipindi kifupi tangu ateuliwe lakini amekuwa mstari wa mbele katika kutatua kero, migogoro, changamoto za wananchi na hasa kupitia kuundwa kwa baraza hili amekuwa DC wa kwanza kuheshimu miongozo ya Serikali kwa kiwango cha juu sana na kuanzisha jukwaa hili la kuhabalishana mawazo na kusaidia ukuaji wa uchumi katika Wilaya yetu ya Magu.
Wajumbe wa Baraza wamesahuri Serikali kuondoa vikwazo kwa wafanya biashara ili waweze kuvutiwa katika uwekezaji. Pia kuchangamkia fursa kwa kuboresha kituo cha makumbusho ya kihistoria cha Kageye, na kujitahidi kujenga vyuo vya ufundi ili kuwezesha ujuzi na teknolojia kwa wananchi waweze kuwekeza kwa tija zaidi, aidha baraza limependekeza kuweka mkazo katika utoaji wa elimu ya ujasiliamali kupitia idara ya Maendeleo ya jamii ambayo imeasahaulika kwa kutopatiwa bajeti ya kutosha kinachopelekea kushindwa kutekeleza majukumu yake ipasavyo.
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Magu. Haki zote zimehifadhiwa