Baraza la wafanyakazi Magu limepitia rasimu ya mpango wa bajeti kwa mwaka 2021/2022 leo tarehe 18.02.2021 katika ukumbi wa Shule ya sekondari Magu. Akifungua baraza hilo la wafanyakazi Mwenyekiti wa kikao ambae pia ni Mkurugenzi Mtendaji (W) amewaruhusu wajumbe kuchangia hoja kuhusiana na Rasimu ya mpango wa Bajeti ambapo fedha zilizoidhinishwa kutumika katika mishahara ya watumishi kwa mwaka 2021/2022 ni jumla ya Tshs. 34,766,354,500.00. Wajumbe wamepitisha rasimu hiyo ya mpango wa bajeti kama ilivyopangwa.
Aidha Afisa Kazi Mkoa wa Mwanza amesimamia uundaji wa Baraza za jipya la wafanyakazi sambamba na kuchagua Makatibu wa Baraza litakalodumu kwa muda wa miaka 3 ambapo ameeleza idadi ya wajumbe wanaohitajika katika Baraza la Wafanyakazi na umuhimu wa Baraza katika Halmashauri.
“Baraza la wafanyakazi limeanzishwa kisheria hivyo kila mahali pa kazi lazima kuwepo na Baraza kulingana na sheria ya ajira na mahusiano maeneo ya kazi, kujenga jamii isiyokuwa na matabaka katika uendeshaji wa taasisi, kuakisi shughuli zinazofanywa na Halmashauri, kuongezea wafanyakazi maarifa kwa sababu ya kushirikishwa kikamilifu, kupunguza migogoro mahali pa kazi na kuwezesha watumishi kutumia vipaji vyao” amesema Afisa kazi.
Pia ameeleza umuhimu wa vikao katika baraza kuwa ni pamoja na kujadili na kufikia mwafaka, mahali pa kupumulia watumishi, kushauri serikali kuhusu sera na kushauri uongozi wa taasisi husika.
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Magu. Haki zote zimehifadhiwa