Baraza la madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Magu limepitisha kwa kauli moja mapendekezo ya rasimu ya mpango na bajeti kwa mwaka wa fedha 2024/2025 ambapo Halmashauri Ya Wilaya ya Magu iliomba kuidhinishiwa jumla ya Sh Bilioni 65 ( 65,039,205,291.04) kutoka vyanzo vyake mbalimbali na kutoka ruzuku ya Serikali kuu.
Akiwasilisha rasimu ya mpango wa bajeti kwa mwaka fedha 2024/2025 Kaimu Afisa mipango Wilaya ya Magu, Christa D. Manyala alitaja jumla ya Tsh. Bilioni 65 ( 65,039,205,291.04) kati ya fedha hizo Bilioni 1.4 ( 1,492,740,064.00) mapato ya ndani, Bilioni 3.2 (3, 223,327,677.04) za matumizi mengineyo, Milioni 10.5 (10,536,000.oo) za mishahara kutoka mapato yandani, Bilioni 45.8 (45,820,693,800.00) ruzuku ya mishahara, Bilioni 13. (1,310,320,000.00) matumizi mengineyo Bilioni 7.2 ( 7,210,144,000.00 miradi ya maendeleo ya serikali na Bilioni 5.9 ( 5, 971,443,759.00) miradi ya maendeleo ya wahisani ambapo jumla kuu ni shilingi Bilioni 65.
Amesema bajeti kuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Magu kwa mwaka wa fedha 2024/2025 imeongezeka kwa asilimia 20 na mapato ya ndani yameongezeka kwa asilimia 3.10 ukilinganisha na bajeti ya mwaka 2023/2024.
Kwa upande wake Mweneykiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Magu Simon Mpandalume amemshukuru Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh. Dkt. Samia Suluhu Hasssan kwa kuendelea kupeleka fedha nyingi kwaajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo katika Wilaya hiyo ikiwemo ujenzi wa shule mpya , zahanati na barabara ambazo zimekua chachu ya maendeleo katika Wilaya ya Magu.
Naye Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Magu Bi. Fidelica Myovella amesema vipaumbele vya bajeti kwa mwaka wa fedha 2024/2025 vitazingatia mwongozo uliotolewa na kuvitaja vipaumbele vya Halmashauri katika bajeti hiyo ambavyo ni kuboresha huduma za afya, kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunza na kuongeza ufanisi na utendaji kazi.
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Magu. Haki zote zimehifadhiwa