• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
    • Malalamiko |
MAGU DISTRICT COUNCIL
MAGU DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Magu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Orodha ya viongozi Waliopita
      • Wenyeviti wa Halmashauri
      • Wakurugenzi
      • Wakuu Wa Wilaya
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Ardhi na Maliasili
      • Kilimo , umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Utumishi na utawala
      • Idara ya Mipango
      • Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Ujenzi
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Fedha
    • Vitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Ugavi
      • Kitengo cha Tehama
      • Internal Audit Unit
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kivutio cha Utalii
      • Bujora
    • Miundombinu ya Umwagiliaji
  • Huduma
    • Afya
    • Maji
    • Elimu
    • Kilimo
  • Madiwani
    • Baraza la Madiwani
      • Wajumbe wa Baraza la Madiwani
      • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Kamati ya fedha, Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya Uchumi Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya UKIMWI (CMAC)
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba ya vikao vya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Maeneo ya uwekezaji
    • Bajeti
      • 2016/2017 Budget
    • TASAF
    • Mpango Mkakati
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • sheria
    • Fomu mbalimbali
    • Zabuni
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • video
    • Hotuba
    • Picha
    • Habari

WALIMU WAASWA KUACHA KUKOPA MIKOPO YA KAUSHA DAMU

Posted on: June 5th, 2024

Na Yusuph Digossi- Magu Dc


MKURUGENZI wa Elimu TAMISEMI Dkt Emmanuel Selemani Shindika  ambaye anashughulikia masuala ya elimu na utawala amewaasa walimu kuacha kukopa mikopo kausha damu kwani  kupitia mikopo hiyo inapelekea walimu kutofundisha kwa weledi na matokeo yake kupelekea kufeli kwa wanafunzi.


Dkt. Shindika ameyasema hayo kwenye kikao cha pamoja na walimu wa shule za Msingi na Sekondari wa Halmashauri ya Wilaya ya Magu kilichofanyika leo (05.06.2024) katika ukumbi wa CCM Wilaya ya Magu.



Amesema baadhi ya walimu wanasalimisha hadi kadi zao za benki kwenye taasisi za fedha ili kukopa fedha zinazowalipisha riba kubwa jambo ambalo linapelekea wengi wao kua na msongo wa mawazo ambao huathiri utendaji wao wa kazi.


Alisema inafikirisha mno kuona mwalimu ana madeni mengi na makubwa kiasi hicho lakini bado serikali na jamii inamtegemea afundishe vizuri na kwa weledi ili kumpa matokeo chanya wanafunzi.


Akifikisha Salamu za Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh. Dkt. Samia Suluhu amesema Rais  anawapenda Walimu na anajua ndiyo nguzo ya Taifa hili na kwamba atawatimizia changamoto zinazo wakabili walimu ikiwa ni pamoja na kupanda vyeo,likizo,malimbikizo ya mishahara,kubadilishwa miundo pamoja na uhamisho.


Aliongeza kuwa hadi kufikia 01,Julai,2024 walimu 54 elfu watapanda vyeo kwa mserereko na Walimu 52 elfu watapanda madaraja kwa utaratibu wa kawaida na kubainisha kuwa madai na changamoto zote za walimu zitafanyiwa kazi.


Afisa Elimu Mkoa wa Mwanza, Martin Nkwabi amesema kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Magu imekuwa ikifanya vizuri kwenye taaluma pamoja na ujenzi wa miundombinu mbalimbali ya sekta ya elimu.


Naye Kaimu Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Magu Henryh Sedatale amesema Wilaya itaendelea kusimamia taaluma kwa kuzingatia ufaulu wa wanafunzi pamoja na ujenzi wa miradi ya elimu na usimamizi wa fedha zote za sekta ya elimu wilayani magu.

Matangazo

  • TANGAZO LA MAJINA YA WAANDISHI NA WAENDESHA VIFAA WALIOTEULIWA KATIKA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA AWAMU YA II April 28, 2025
  • TANGAZO LA UUZAJI WA VIWANJA HALMASHAURI YA WILAYA YA MAGU ENEO LA ILUNGU NA IGUDIJA TAREHE 02/12/2024 December 01, 2024
  • TANGAZO KWA UMMA November 18, 2022
  • FOMU ZA KUJIUNGA SHULE YA WASICHANA YA MKOA WA MWANZA MWANZA GIRLS SS 2023 December 16, 2022
  • Angalia zote

Habari mpya

  • WANANCHI NYASHIMBA WAISHUKURU HALMASHAURI MAGU UJENZI WA ZAHANATI, SHULE

    June 13, 2025
  • MAGU YATENGENEZA MADAWATI 1300 KWA FEDHA ZA MAPATO YA NDANI

    June 12, 2025
  • MILIONI 250 ZA MFUKO WA JIMBO ZAACHA ALAMA MAGU

    June 09, 2025
  • WAKULIMA MAGU WAMPA TANO KISWAGA KUCHOCHEA KILIMO CHA UMWAGILIAJI

    June 07, 2025
  • Angalia zote

Video

Serikali yatoa Matrekata 33 katika Halmashauri ya Wilaya ya Magu
More Videos

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Ugonjwa
  • Fomu ya Kusafiri nje ya Kituo cha kazi
  • Sheria ndogo za Halmashauri
  • Fomu ya Opras
  • Fomu Mpya ya Maombi ya Likizo kwa watumishi
  • Fomu ya Quotation ya likizo
  • Taratibu za mikutano na uendeshaji shughuli za Halmashauri
  • Mwongozo wa Uwekezaji Mkoa wa Mwanza
  • Utaratibu wa kutoa Leseni ya Biashara

Viunganishi Linganifu

  • Wakala ya Serikali Mtandao.
  • Wizara ya Afya
  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti kuu ya serikali
  • Ofisi ya Taifa ya takwimu Tanzania
  • tovuti ya Ikulu
  • Tovuti ya Mkoa wa Mwanza

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Magu. Haki zote zimehifadhiwa