ALIYEKUWA Katibu Tawala ya Wilaya ya Magu -DAS, Jubilate Win Lauwo leo Jumanne tarehe 1 Julai, 2025 amekabidhi ofisi kwa Zuberi Said Zuberi na kumuahidi ushirikiano wa kutosha katika nafasi yake hiyo mpya.
Bi. Lauwo ambaye pia wiki iliyopita Rais Samia Suluhu Hassan ameteua kuwa mkuu wa wilaya hiyo ya Magu, amekaribisha DAS Zuberi na kumpongeza katika nafasi hiyo ambayo inaonesha ameaminiwa pakubwa na Rais Samia.
Akizungumza baada ya kukabidhiwa ofisi Zuberi amewataka watumishi wa ofisi hiyo kuzingatia maadili na nidhamu katika utekelezaji wa majukumu yao.
Aidha, mbali na kumpongeza Bi. Lauwo kwa uteuzi wa DC wa wilaya hiyo, pia amemshukuru Rais Samia kwa kumuona na kumteua kuwa DAS wa wilaya hiyo kutoka kuwa mtendaji wa moja ya kata za wilaya ya Tunduru.
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Magu. Haki zote zimehifadhiwa