• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
    • Malalamiko |
MAGU DISTRICT COUNCIL
MAGU DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Magu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Orodha ya viongozi Waliopita
      • Wenyeviti wa Halmashauri
      • Wakurugenzi
      • Wakuu Wa Wilaya
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Ardhi na Maliasili
      • Kilimo , umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Utumishi na utawala
      • Idara ya Mipango
      • Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Ujenzi
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Fedha
    • Vitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Ugavi
      • Kitengo cha Tehama
      • Internal Audit Unit
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kivutio cha Utalii
      • Bujora
    • Miundombinu ya Umwagiliaji
  • Huduma
    • Afya
    • Maji
    • Elimu
    • Kilimo
  • Madiwani
    • Baraza la Madiwani
      • Wajumbe wa Baraza la Madiwani
      • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Kamati ya fedha, Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya Uchumi Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya UKIMWI (CMAC)
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba ya vikao vya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Maeneo ya uwekezaji
    • Bajeti
      • 2016/2017 Budget
    • TASAF
    • Mpango Mkakati
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • sheria
    • Fomu mbalimbali
    • Zabuni
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • video
    • Hotuba
    • Picha
    • Habari

Naibu Waziri Awataka Wakuu wa Wilaya Kuchukua Hatua kwa Wakopeshaji waliochukua Kadi za Watumishi

Posted on: March 2nd, 2020

Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Mheshimiwa Josephat Kandege amesema hayo kwenye ziara  aliyofanya wilayani Magu tarehe 28.02. 2020 wakati akizungumza na watumishi wa Umma katika ukumbi wa Shule ya sekondari Magu. Amesema kuwa wakopeshaji hao wasio rasmi  wamekuwa wakichukua kadi za watumishi na kutumia mikataba ya ulaghai.

Amepongeza Halmashauri ya Magu  kupeleka watumishi 6 wa Idara ya afya masomoni, kuanzisha mfuko wa elimu, kufanya vizuri katika matokeo ya darasa la saba na kidato cha sita na walimu waliojitolea kujenga darasa kwa fedha zao ambapo amesema kuwa huo ni uzalendo mkubwa ulioonyeshwa na walimu hao.

Aidha  amesema “ili Halmashauri ipate maendeleo watumishi lazima wapate ari ya kufanya kazi kwa bidii na ili Halmashauri iweze kujiendesha  Lazima kuzingatia ukusanyaji wa Mapato na watendaji wa Kata na vijiji wawe wasimamizi kuhakikisha mapato ya Halmashauri yanakusanywa” amesema Naibu waziri OR-TAMISEMI.

Awali Mkuu wa Wilaya ya Magu Dkt Philemon Sengati amemshukuru Naibu Waziri kutembelea Magu na kuzungumza na watumishi, “Magu tumeamua kufanya kazi kwa uzalendo mkubwa na mshikamano na tunazingatia rasilimali watu” amesema Dkt Sengati.

Mbunge  Jimbo la Magu Mhe. Destery Kiswaga amesema kuwa watumishi wana changamoto nyingi serikali ikiendelea kuzipunguza watakuwa na molari ya kufanya kazi. Pia Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe Hilali Elisha  amesema wananchi wa Magu wamehamasika sana katika kuinua maboma ya Madarasa na zahanati katika suala la kuleta maendeleo ameomba serikali kusaidia nguvu za wananchi kwa kuezeka maboma yaliyopo.

Mkurugenzi Mtendaji Wilaya Bw Lutengano G. Mwalwiba amesema kuwa serikali imeendelea kushughulikia changamoto za watumishi kwa wakati kwani changamoto kubwa iliyopo ni upandishaji wa madaraja kwa watumishi. Mwaka 2019 serikali ilitoa kibari cha kupandisha watumishi lakini waliobadilishiwa mshahara ni watumishi 411 bado watumishi 74 ambao hawajabadilishiwa mshahara hivyo ameomba Serikali kuwabadilishia mshahara watumishi waliobaki katika Halmashauri ya Magu.

Matangazo

  • TANGAZO LA MAJINA YA WAANDISHI NA WAENDESHA VIFAA WALIOTEULIWA KATIKA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA AWAMU YA II April 28, 2025
  • TANGAZO LA UUZAJI WA VIWANJA HALMASHAURI YA WILAYA YA MAGU ENEO LA ILUNGU NA IGUDIJA TAREHE 02/12/2024 December 01, 2024
  • TANGAZO KWA UMMA November 18, 2022
  • FOMU ZA KUJIUNGA SHULE YA WASICHANA YA MKOA WA MWANZA MWANZA GIRLS SS 2023 December 16, 2022
  • Angalia zote

Habari mpya

  • WANANCHI NYASHIMBA WAISHUKURU HALMASHAURI MAGU UJENZI WA ZAHANATI, SHULE

    June 13, 2025
  • MAGU YATENGENEZA MADAWATI 1300 KWA FEDHA ZA MAPATO YA NDANI

    June 12, 2025
  • MILIONI 250 ZA MFUKO WA JIMBO ZAACHA ALAMA MAGU

    June 09, 2025
  • WAKULIMA MAGU WAMPA TANO KISWAGA KUCHOCHEA KILIMO CHA UMWAGILIAJI

    June 07, 2025
  • Angalia zote

Video

Serikali yatoa Matrekata 33 katika Halmashauri ya Wilaya ya Magu
More Videos

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Ugonjwa
  • Fomu ya Kusafiri nje ya Kituo cha kazi
  • Sheria ndogo za Halmashauri
  • Fomu ya Opras
  • Fomu Mpya ya Maombi ya Likizo kwa watumishi
  • Fomu ya Quotation ya likizo
  • Taratibu za mikutano na uendeshaji shughuli za Halmashauri
  • Mwongozo wa Uwekezaji Mkoa wa Mwanza
  • Utaratibu wa kutoa Leseni ya Biashara

Viunganishi Linganifu

  • Wakala ya Serikali Mtandao.
  • Wizara ya Afya
  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti kuu ya serikali
  • Ofisi ya Taifa ya takwimu Tanzania
  • tovuti ya Ikulu
  • Tovuti ya Mkoa wa Mwanza

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Magu. Haki zote zimehifadhiwa