HALMASHAURI ya Wilaya ya Magu imekabidhi madawati 1300 kwa shule 59 zilizopo wilayani humo ambapo shule za msingi 56 na sekondari 3 zimekabidhiwa madawati hayo yaliyotengenezwa na halmashauri kwa kutumia mapato ya ndani.
Akizungumza wakati akikabidhi madawati hayo kwa niaba ya mwenyekiti wa halmashauri, Simon Mpandalume, Diwani wa kata ya Sukuma na mwenyekiti wa kamati ya elimu afya na maji, Faustine Makingi amesema madawati hayo yametengenezwa kwa kiasi cha shilingi milioni 92 za mapato ya ndani ambazo zilitengwa kwaajili ya shuguli hiyo.
Akizungumza kwa niaba ya mkurugenzi mtendaji, Mohamed Ramadhani, Afisa utumishi wa Wilaya ya Magu, Henry Sedatale amesema madawati hayo yatasambazwa kwenye shule za msingi na sekondari zenye uhaba wa samani hizo Pamoja na shule mpya zinazotarajiwa kufunguliwa wilayani hapa.
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Magu. Haki zote zimehifadhiwa