• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
    • Malalamiko |
MAGU DISTRICT COUNCIL
MAGU DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Magu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Orodha ya viongozi Waliopita
      • Wenyeviti wa Halmashauri
      • Wakurugenzi
      • Wakuu Wa Wilaya
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Ardhi na Maliasili
      • Kilimo , umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Utumishi na utawala
      • Idara ya Mipango
      • Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Ujenzi
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Fedha
    • Vitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Ugavi
      • Kitengo cha Tehama
      • Internal Audit Unit
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kivutio cha Utalii
      • Bujora
    • Miundombinu ya Umwagiliaji
  • Huduma
    • Afya
    • Maji
    • Elimu
    • Kilimo
  • Madiwani
    • Baraza la Madiwani
      • Wajumbe wa Baraza la Madiwani
      • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Kamati ya fedha, Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya Uchumi Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya UKIMWI (CMAC)
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba ya vikao vya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Maeneo ya uwekezaji
    • Bajeti
      • 2016/2017 Budget
    • TASAF
    • Mpango Mkakati
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • sheria
    • Fomu mbalimbali
    • Zabuni
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • video
    • Hotuba
    • Picha
    • Habari

DC Magu azindua Kampeni ya Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto

Posted on: September 30th, 2019

Mkuu wa Wilaya ya Magu Dr. Philemon Sengati amezindua Kampeni ya kutokomeza Ukatili dhidi ya wanawake na watoto, uzinduzi huo umefanyika katika viwanja vya Sabasaba vilivyopo kata ya Magu Mjini  leo tarehe 30.09.2019. Amesema  kuwa, Msingi wa kampeni hizi zinazo zinduliwa leo zinatokana na kuwepo kwa Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA-2017/18-2021/22) ambao ni mpango kazi wa miaka mitano ulio andaliwa na serikali lengo kuu likiwa ni kutokomeza au kumaliza kabisa ukatili dhidi ya wanawake na watoto katika nchi yetu ya Tanzania.

“Jamii zetu lazima zitambue kuwa Wilaya yetu ya Magu haipo salama kwa kuwa matendo ya ukatili yapo na yanatokea kila siku. Ni jukumu la kila mmoja sasa kuchukua hatua za kukomesha kabisa vitendo vya ukatili vinavyofanywa kwa wanawake na watoto” amesema Dr. Sengati.

Ameendelea kusema kwamba, Halmashauri ya wilaya ya Magu itaendelea kulinda na kutetea haki za wanawake na watoto ikiwa ni pamoja kuelimisha jamii kuwajibika ipasavyo katika  kuwasaidia na kuwahudumia waathirika wa ukatili. “Pia niwaombe viongozi ngazi zote kwa kushirikiana na Halmashauri kutoa taarifa na kuchukua hatua za haraka pale haki za wanawake na watoto zinapokiukwa pamoja na haki za watu wengine katika jamii”.

“Niwaombe wananchi wote kuanzia ngazi ya vitongoji, vijiji, kata, viongozi wa madhehebu ya dini, viongozi wa vyama vya siasa na kila mtu kwa nafasi yake tuendelee kulaani na kukumea kwa nguvu zetu zote vitendo vyote vya ukatili vinavyotokea katika maeneo yetu” amesema Dr Sengati.

 Aidha DC ametoa shukurani kwa shirika la KIVULINI ambalo limekuwa mstari wambele kufanya kazi kwa ushirikiano mkubwa na Serikali kuhakikisha jamii yetu ya Magu na Tanzania kwa ujumla inakuwa salama na jamii inaishi kwa amani na upendo na ikiondokana na vitendo vya ukatili vinavyorudisha nyuma maendeleo na kuwanyima watu haki zao za msingi zikiwemo haki ya kuishi, kupata elimu, haki ya kusikilizwa, haki ya kuthaminiwa na nyingine nyingi.

“Lakini nitumie fursa hii kuwashukuru walioandaa uzinduzi huu ikiwa ni pamoja na uongozi wa kata zote tatu za hapa mjini ambazo ni Magu mjini, Isandula na Itumbili. Sambamba na hilo niipongeze Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa wilaya kwa kuratibu shughuli hii muhimu kupitia kwa maafisa  walio chini yake ambao ni kitengo cha ustawi wa jamii, Idara ya Elimu Msingi na Sekondari, Idara ya maendeleo ya Jamii, Idara ya Afya nanyi nginezo. Hongereni sana, kazi yenu ni njema. Aidha nawapongeza wadau wengine wote walioshiriki likiwemo Jeshi la polisi, mahakama ya Wilaya kufanikisha shughuli hii muhimu. Kwa namna ya pekee niwashukuru wananchi wote waliotoka sehemu mbalimbali za wilaya yetu kuja kushiriki katika siku hii maalumu.

“Magu ni Kusema na Kutenda, Kazi kwa Maendeleo”

Matangazo

  • TANGAZO LA MAJINA YA WAANDISHI NA WAENDESHA VIFAA WALIOTEULIWA KATIKA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA AWAMU YA II April 28, 2025
  • TANGAZO LA UUZAJI WA VIWANJA HALMASHAURI YA WILAYA YA MAGU ENEO LA ILUNGU NA IGUDIJA TAREHE 02/12/2024 December 01, 2024
  • TANGAZO KWA UMMA November 18, 2022
  • FOMU ZA KUJIUNGA SHULE YA WASICHANA YA MKOA WA MWANZA MWANZA GIRLS SS 2023 December 16, 2022
  • Angalia zote

Habari mpya

  • WANANCHI NYASHIMBA WAISHUKURU HALMASHAURI MAGU UJENZI WA ZAHANATI, SHULE

    June 13, 2025
  • MAGU YATENGENEZA MADAWATI 1300 KWA FEDHA ZA MAPATO YA NDANI

    June 12, 2025
  • MILIONI 250 ZA MFUKO WA JIMBO ZAACHA ALAMA MAGU

    June 09, 2025
  • WAKULIMA MAGU WAMPA TANO KISWAGA KUCHOCHEA KILIMO CHA UMWAGILIAJI

    June 07, 2025
  • Angalia zote

Video

Serikali yatoa Matrekata 33 katika Halmashauri ya Wilaya ya Magu
More Videos

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Ugonjwa
  • Fomu ya Kusafiri nje ya Kituo cha kazi
  • Sheria ndogo za Halmashauri
  • Fomu ya Opras
  • Fomu Mpya ya Maombi ya Likizo kwa watumishi
  • Fomu ya Quotation ya likizo
  • Taratibu za mikutano na uendeshaji shughuli za Halmashauri
  • Mwongozo wa Uwekezaji Mkoa wa Mwanza
  • Utaratibu wa kutoa Leseni ya Biashara

Viunganishi Linganifu

  • Wakala ya Serikali Mtandao.
  • Wizara ya Afya
  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti kuu ya serikali
  • Ofisi ya Taifa ya takwimu Tanzania
  • tovuti ya Ikulu
  • Tovuti ya Mkoa wa Mwanza

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Magu. Haki zote zimehifadhiwa