Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene, amefanya ziara ya kutembelea mradi wa Nyumba za Makazi zilizojengwa na Watumishi Housing Investments (WHI) katika eneo la Isangijo, Kata ya Bukandwe Wilayani Magu Mkoani Mwanza.
Baada ya kutembelea mradi huo Mhe.Simbachawene ameipongeza Watumishi Housing kwa kutekeleza mradi huo wenye jumla ya Nyumba 59 ambapo nyumba 20 zimenunuliwa na nyumba 39 kupangishwa kwa watumishi wa Umma.
Aidha Mhe.Simbachawene ameagiza kuendelea kutafuta viwanja katika maeneo mbali mbali Nchini kwa kusjirikiana na mamlaka husika maeneo hayo ili kutimiza lengo la Taasisi hiyo ambalo ni kutoa huduma ya Makazi Bora na kwa Bei nafuu kwa Watumishi wa umma, wafanyakazi wa sekta binafsi pamoja na wanachama wote wa mifuko ya hifadhi ya jamii.
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Magu. Haki zote zimehifadhiwa