• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
    • Malalamiko |
MAGU DISTRICT COUNCIL
MAGU DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Magu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Orodha ya viongozi Waliopita
      • Wenyeviti wa Halmashauri
      • Wakurugenzi
      • Wakuu Wa Wilaya
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Ardhi na Maliasili
      • Kilimo , umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Utumishi na utawala
      • Idara ya Mipango
      • Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Ujenzi
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Fedha
    • Vitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Ugavi
      • Kitengo cha Tehama
      • Internal Audit Unit
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kivutio cha Utalii
      • Bujora
    • Miundombinu ya Umwagiliaji
  • Huduma
    • Afya
    • Maji
    • Elimu
    • Kilimo
  • Madiwani
    • Baraza la Madiwani
      • Wajumbe wa Baraza la Madiwani
      • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Kamati ya fedha, Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya Uchumi Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya UKIMWI (CMAC)
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba ya vikao vya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Maeneo ya uwekezaji
    • Bajeti
      • 2016/2017 Budget
    • TASAF
    • Mpango Mkakati
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • sheria
    • Fomu mbalimbali
    • Zabuni
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • video
    • Hotuba
    • Picha
    • Habari

WAZIRI MKUU AKAGUA MAENDELEO MRADI WA MAJI BUJORA-KISESA WILAYANI MAGU

Posted on: December 21st, 2024

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Desemba 21, 2024 amewasili mkoani Mwanza kwa ziara ya kikazi na kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa tenki la kuhifadhi maji la Bujora – Kisesa lililoyopo wilayani Magu mkoani Mwanza ikiwa ni mpango wa muda wa kati wa kuboresha huduma ya maji Mwanza ambao unatarajiwa kugharimu shilingi bilioni 3.54.

Mradi huo ambao unafadhiliwa na Serikali ya Tanzania na Shirika la Maendeleo la Ufaransa (France Development Agency) hadi kukamilika kwake na mpaka sasa umefikia asilimia 93 na unatarajiwa kuhudumia wananchi 75,000 wa maeneo ya maeneo ya Kisesa, Bujora, Igudija na sehemu za jirani.

Akizungumza na wananchi wa eneo la Bujora baada ya kukagua mradi huo Majaliwa amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imefanya kazi kubwa ya utekelezaji wa miradi mikubwa inayowagusa wananchi moja kwa moja kwenye sekta za elimu, afya, maji, kilimo, uvuvi na barabara.

Kwa Upande wake, Waziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema wizara hiyo itaendelea kusimamia maagizo ya Rais Dkt. Samia ya kuhakikisha wananchi wanapata maji katika maeneo yao.

“Mheshimiwa Rais Dkt. Samia alisema hataki kuona wananchi wanateseka kutafuta maji,” amesema.

Naye Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mwanza (MWAUWASA), Nelly Msuya amesema kuwa Matenki mengine yatajengwa katika maeneo ya vilima vinavyozunguka Mji wa Mwanza ikiwemo Nyamazobe (lita milioni 10), Buhongwa (Lita milioni 5), Fumagila (Lita milioni 10) na Usagara (lita milioni 1).

“Utekelezaji wa mradi huu wa thamani ya Tsh. Bilioni 49 umeanza na unatarajiwa kukamilika ndani ya miaka miwili (2) ifikapo Desemba 2026,” amesema.

Aidha, amesema kuwa ujenzi wa tenki la Bujora - Kisesa lenye ujazo wa lita milioni 5, unatarajiwa kukamilika ifikapo Februari, 2025.

Matangazo

  • TANGAZO LA MAJINA YA WAANDISHI NA WAENDESHA VIFAA WALIOTEULIWA KATIKA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA AWAMU YA II April 28, 2025
  • TANGAZO LA UUZAJI WA VIWANJA HALMASHAURI YA WILAYA YA MAGU ENEO LA ILUNGU NA IGUDIJA TAREHE 02/12/2024 December 01, 2024
  • TANGAZO KWA UMMA November 18, 2022
  • FOMU ZA KUJIUNGA SHULE YA WASICHANA YA MKOA WA MWANZA MWANZA GIRLS SS 2023 December 16, 2022
  • Angalia zote

Habari mpya

  • WADAU WA SANAA MAGU WATAKIWA KUJISAJILI BASATA

    May 07, 2025
  • INEC YARIDHISHWA UBORESHAJI DAFTARI LA WAPIGA KURA MAGU

    May 03, 2025
  • DC Magu:Wazazi pelekeni watoto wapate chanjo ya polio

    April 30, 2025
  • WAANDISHI, WAENDESHA BVR 136 WALA KIAPO MAGU

    April 29, 2025
  • Angalia zote

Video

Serikali yatoa Matrekata 33 katika Halmashauri ya Wilaya ya Magu
More Videos

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Ugonjwa
  • Fomu ya Kusafiri nje ya Kituo cha kazi
  • Sheria ndogo za Halmashauri
  • Fomu ya Opras
  • Fomu Mpya ya Maombi ya Likizo kwa watumishi
  • Fomu ya Quotation ya likizo
  • Taratibu za mikutano na uendeshaji shughuli za Halmashauri
  • Mwongozo wa Uwekezaji Mkoa wa Mwanza
  • Utaratibu wa kutoa Leseni ya Biashara

Viunganishi Linganifu

  • Wakala ya Serikali Mtandao.
  • Wizara ya Afya
  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti kuu ya serikali
  • Ofisi ya Taifa ya takwimu Tanzania
  • tovuti ya Ikulu
  • Tovuti ya Mkoa wa Mwanza

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Magu. Haki zote zimehifadhiwa