• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
    • Malalamiko |
MAGU DISTRICT COUNCIL
MAGU DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Magu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Orodha ya viongozi Waliopita
      • Wenyeviti wa Halmashauri
      • Wakurugenzi
      • Wakuu Wa Wilaya
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Ardhi na Maliasili
      • Kilimo , umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Utumishi na utawala
      • Idara ya Mipango
      • Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Ujenzi
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Fedha
    • Vitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Ugavi
      • Kitengo cha Tehama
      • Internal Audit Unit
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kivutio cha Utalii
      • Bujora
    • Miundombinu ya Umwagiliaji
  • Huduma
    • Afya
    • Maji
    • Elimu
    • Kilimo
  • Madiwani
    • Baraza la Madiwani
      • Wajumbe wa Baraza la Madiwani
      • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Kamati ya fedha, Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya Uchumi Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya UKIMWI (CMAC)
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba ya vikao vya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Maeneo ya uwekezaji
    • Bajeti
      • 2016/2017 Budget
    • TASAF
    • Mpango Mkakati
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • sheria
    • Fomu mbalimbali
    • Zabuni
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • video
    • Hotuba
    • Picha
    • Habari

WANANCHI NYASHIMBA WAISHUKURU HALMASHAURI MAGU UJENZI WA ZAHANATI, SHULE

Posted on: June 13th, 2025

WANANCHI wa Kijiji cha Nyashimba katika Halmashauri ya Wilaya ya Magu mkoani Mwanza wameushukuru uongozi wa hamshauri hiyo kwa kuwajengea zahanati ya pamoja na shule ya sekondari hali itakayochochea maendeleo ya sekta ya afya na elimu kijijini hapo.

Hayo yamebainishwa jana Alhamisi tarehe 12 Juni 2025 katika ziara ya Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Simon Mpandalume ambaye pia ni Diwani wa kata ya Nyigogo.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi wananchi hao akiwamo Elizabeth Komba amesema ujenzi wa zahanati hiyo utakuwa mkombozi kwa wakati wa Kijiji hicho hasa ikizingatiwa wakazi wake walikuwa wanatembea umbali mrefu kufuata huduma katika hospitali ya wilaya.

“Lakini zahanati hii ikikamilika hakika akina mama hawatapa tena shida ya kujifungua kwani huduma watapata hapa na hata baada ya muda tunatarajia itapandishwa hadhi kuwa kituo cha afya.

“Kuhusu shule ya sekondari Nyashimba pia itawasaidia Watoto wetu kuepukana na vishawishi mbalimbali walivyokuwa wanakumbana navyo pindi wanapoenda shule jirani za Kinango,” amesema Elizabeth na kuungwa mkono na Mchunga Hernest Cherehani ambaye amesema ujio wa miradi hiyo imekuwa chachu kwa wananchi kuendelea kuhamasisha kuchangia miradi ya maendeleo.

Awali akizungumza na wananchi hao na kuwashukuru kwa kumpa nafasi ya kuwaongoza kwa miaka mitano, Mpandalume amesema miradi hiyo inatekelezwa kwa mapato ya ndani ya halmashauri pamoja na nguvu za wadau akiwamo mbunge wa Magu, Boniventura Kiswaga.

Amesema zahanati hiyo ambayo ilianza kujengwa mwaka 2020, imetumia zaidi ya Sh milioni 45 fedha za mapato ya ndani ya halmashauri huku mbunge akichangia saruji mifuko 150.

Aidha, ameahidi kumalizia ujenzi wa zahanati hiyo ambapo halmashauri itatoa tena Sh milioni 35 ambapo hadi kufikia Agosti mwaka huu ujenzi huo utakamilika na mradi kuzinduliwa na kiongozi wa mbio za mwenge wa Uhuru.

Kwa upande wa mradi wa shule ya sekondari tayari ulioanza 2020/2021 hadi sasa umefikia hatua nzuri huku kazi iliyobaki ikiwa ni kukamilisha ujenzi wa vyoo.

Matangazo

  • TANGAZO LA MAJINA YA WAANDISHI NA WAENDESHA VIFAA WALIOTEULIWA KATIKA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA AWAMU YA II April 28, 2025
  • TANGAZO LA UUZAJI WA VIWANJA HALMASHAURI YA WILAYA YA MAGU ENEO LA ILUNGU NA IGUDIJA TAREHE 02/12/2024 December 01, 2024
  • TANGAZO KWA UMMA November 18, 2022
  • FOMU ZA KUJIUNGA SHULE YA WASICHANA YA MKOA WA MWANZA MWANZA GIRLS SS 2023 December 16, 2022
  • Angalia zote

Habari mpya

  • WANANCHI NYASHIMBA WAISHUKURU HALMASHAURI MAGU UJENZI WA ZAHANATI, SHULE

    June 13, 2025
  • MAGU YATENGENEZA MADAWATI 1300 KWA FEDHA ZA MAPATO YA NDANI

    June 12, 2025
  • MILIONI 250 ZA MFUKO WA JIMBO ZAACHA ALAMA MAGU

    June 09, 2025
  • WAKULIMA MAGU WAMPA TANO KISWAGA KUCHOCHEA KILIMO CHA UMWAGILIAJI

    June 07, 2025
  • Angalia zote

Video

Serikali yatoa Matrekata 33 katika Halmashauri ya Wilaya ya Magu
More Videos

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Ugonjwa
  • Fomu ya Kusafiri nje ya Kituo cha kazi
  • Sheria ndogo za Halmashauri
  • Fomu ya Opras
  • Fomu Mpya ya Maombi ya Likizo kwa watumishi
  • Fomu ya Quotation ya likizo
  • Taratibu za mikutano na uendeshaji shughuli za Halmashauri
  • Mwongozo wa Uwekezaji Mkoa wa Mwanza
  • Utaratibu wa kutoa Leseni ya Biashara

Viunganishi Linganifu

  • Wakala ya Serikali Mtandao.
  • Wizara ya Afya
  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti kuu ya serikali
  • Ofisi ya Taifa ya takwimu Tanzania
  • tovuti ya Ikulu
  • Tovuti ya Mkoa wa Mwanza

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Magu. Haki zote zimehifadhiwa