• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
    • Malalamiko |
MAGU DISTRICT COUNCIL
MAGU DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Magu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Orodha ya viongozi Waliopita
      • Wenyeviti wa Halmashauri
      • Wakurugenzi
      • Wakuu Wa Wilaya
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Ardhi na Maliasili
      • Kilimo , umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Utumishi na utawala
      • Idara ya Mipango
      • Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Ujenzi
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Fedha
    • Vitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Ugavi
      • Kitengo cha Tehama
      • Internal Audit Unit
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kivutio cha Utalii
      • Bujora
    • Miundombinu ya Umwagiliaji
  • Huduma
    • Afya
    • Maji
    • Elimu
    • Kilimo
  • Madiwani
    • Baraza la Madiwani
      • Wajumbe wa Baraza la Madiwani
      • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Kamati ya fedha, Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya Uchumi Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya UKIMWI (CMAC)
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba ya vikao vya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Maeneo ya uwekezaji
    • Bajeti
      • 2016/2017 Budget
    • TASAF
    • Mpango Mkakati
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • sheria
    • Fomu mbalimbali
    • Zabuni
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • video
    • Hotuba
    • Picha
    • Habari

TFS MAGU YAGAWA MICHE 200,000 YA MITI KUUNGA MKONO JITIHADA ZA SAMIA UHIFADHI WA MAZINGIRA

Posted on: June 4th, 2025

KATIKA kuunga mkono jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan za kuhamasisha wananchi kutumia nishati safi na kuhifadhi mazingira, Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania katika wilaya ya Magu, umezalisha na kugawa miche ya miti aina tofauti zaidi ya 200,000 kwa wananchi na makundi mbalimbali wilayani huyo.

Pia katika kuadhimisha wiki ya mazingira duniani ambayo kilele chake kinafikiwa tarehe 5 Juni mwaka huu, TFS – Magu imegawa miche ya miti 250 kwa wananchi na shule mbalimbali wilayani humo kwa ajili ya kupanda miti ya kivuli na mtunda na kufikisha idadi ya miche 200,250 iliyogawiwa hadi sasa.

Hayo yamebainishwa leo Jumatano tarehe 4 Juni, 2025 na Afisa uhifadhi misitu II kutoka TFS Magu, Marwa Mshehe wakati akizungumza katika maadhimisho ya siku ya mazingira yaliyofanyika wilayani humo.

Mshehe amesema katika kipindi cha mwaka mmoja tayari wamegawa miche hiyo ya miti kwa makundi mbalimbali ambayo wanaamini imekwenda kuongeza uoto wa asili katika eneo hilo huku jamii ikifaidika kutokana na miche ya miti ya matunda iliyogawiwa pia.

Naye Balozi wa Mazingira Tanzania kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais – Mazingira, Ahidi Sinene ambaye alikuwa mgeni rasmi katika maadhimishi hayo ameupongeza uongozi wa wilaya hiyo kwa kuwa mstari wa mbele kuhamasisha wananchi kupanda miti na kuhifadhi mazingira.

“Tupo kwenye wiki ya mazingira duniani, maadhimisho yake ni tarehe 5 Juni kila mwaka, kwa hiyo ofisi ya Makamu wa Rais tunapita kwa wananchi kuwahasisha kupinga matumizi ya plastiki kwa sababu kwanza ni sumu, ukiitumia binafsi unaenda kufanyiwa operesheni, lakini inaharibu ikolojia ya maji na kudumaza mazao, tunapaswa kupinga matumizi ya plastiki na kutumia mifuko ambayo ni rafiki kwa mazingira yetu,” amesema.

Naye Katibu Tawala wa wilaya hiyo ya Magu, Jubilate Lawuo amesema katika maadhimisho hayo ambayo wamegawa miche ziadi ya 100 kwa wananchi wa shule ya msingi Nyalikungu, Magu imeendelea kuwa mfano wa kuigwa katika kutekeleza mpango wa Rais Samia wa kwa kuwa balozi bora wa mazingira.

“Rais Samia amekuwa balozi wa kwanza katika kuboresha mazingira. Katika kipindi cha miaka mitano amehamasisha wananchi kuachana na kutumia nishati safi na sisi Magu tumefanikiwa kuvutia wadau ambao wamesambaza mitungi ya gesi zaidi ya 3900 kwa akina mama ntilie na watu wa makundi mengine ili waachane na matumizi ya mkaa.

“Nami nimekuwa mstari wa mbele kuadhimishwa siku hii kwa kupanda miti ili kuhamasisha wananchi waendelee kuachana na mkaa ili kuendana na kuli mbiu yam waka huu inayosema “Mazingira yetu na Tanzania ijayo, tudhibiti matumizi ya plastiki,” amesema.

Matangazo

  • TANGAZO LA MAJINA YA WAANDISHI NA WAENDESHA VIFAA WALIOTEULIWA KATIKA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA AWAMU YA II April 28, 2025
  • TANGAZO LA UUZAJI WA VIWANJA HALMASHAURI YA WILAYA YA MAGU ENEO LA ILUNGU NA IGUDIJA TAREHE 02/12/2024 December 01, 2024
  • TANGAZO KWA UMMA November 18, 2022
  • FOMU ZA KUJIUNGA SHULE YA WASICHANA YA MKOA WA MWANZA MWANZA GIRLS SS 2023 December 16, 2022
  • Angalia zote

Habari mpya

  • Shule 53 Magu zagawiwa zana za kufundishia wanafunzi wa awali

    June 05, 2025
  • TFS MAGU YAGAWA MICHE 200,000 YA MITI KUUNGA MKONO JITIHADA ZA SAMIA UHIFADHI WA MAZINGIRA

    June 04, 2025
  • PPRA YAWAPIGA MSASA WALIMU WAKUU, WATENDAJI KATA MAGU KUHUSU MATUMIZI MFUMO NeST

    May 27, 2025
  • Mchengerwa aagiza maofisa habari kukabidhiwa ofisi

    May 23, 2025
  • Angalia zote

Video

Serikali yatoa Matrekata 33 katika Halmashauri ya Wilaya ya Magu
More Videos

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Ugonjwa
  • Fomu ya Kusafiri nje ya Kituo cha kazi
  • Sheria ndogo za Halmashauri
  • Fomu ya Opras
  • Fomu Mpya ya Maombi ya Likizo kwa watumishi
  • Fomu ya Quotation ya likizo
  • Taratibu za mikutano na uendeshaji shughuli za Halmashauri
  • Mwongozo wa Uwekezaji Mkoa wa Mwanza
  • Utaratibu wa kutoa Leseni ya Biashara

Viunganishi Linganifu

  • Wakala ya Serikali Mtandao.
  • Wizara ya Afya
  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti kuu ya serikali
  • Ofisi ya Taifa ya takwimu Tanzania
  • tovuti ya Ikulu
  • Tovuti ya Mkoa wa Mwanza

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Magu. Haki zote zimehifadhiwa