Mkuu wa wilaya ya Magu mh Salum Kalli,mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya bi Fidelica Myovella leo tarehe mosi Desemba wameongoza watumishi na wanachi kushirki katika maadhimisho ya siku ya ukimwi duniani kwa kpanda na kutoa zawadi kwa wagonjwa katika hospitali ya wilaya ya magu
Akizungumza na wananchi walioshiriki na wagonjwa walioshiriki katika maadhimisho hayo mkuu huyo wa wilaya amewaomba wananchi wasiwafiche na kuwabagua wagojwa walipatikana na maambukizi ya ukimwi kwa sasa dawa za kufubaisha virusi zinapatikana
Aidha mkurugenzi mtendaji wa halmashauri bi Fidelica myovella kwa upande wake amewataka wananchi kujishughulisha na ulimaji wa vyakula lishe ikiwa ni Pamoja matunda ambayo yataimarisha kinga katika miili yao akitolea mfano wa mbogamboga viazi lishe ambayo nirahisi kuvitunza kwani havina gharama ya utunzaji wake
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Magu. Haki zote zimehifadhiwa