• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
    • Malalamiko |
MAGU DISTRICT COUNCIL
MAGU DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Magu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Orodha ya viongozi Waliopita
      • Wenyeviti wa Halmashauri
      • Wakurugenzi
      • Wakuu Wa Wilaya
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Ardhi na Maliasili
      • Kilimo , umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Utumishi na utawala
      • Idara ya Mipango
      • Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Ujenzi
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Fedha
    • Vitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Ugavi
      • Kitengo cha Tehama
      • Internal Audit Unit
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kivutio cha Utalii
      • Bujora
    • Miundombinu ya Umwagiliaji
  • Huduma
    • Afya
    • Maji
    • Elimu
    • Kilimo
  • Madiwani
    • Baraza la Madiwani
      • Wajumbe wa Baraza la Madiwani
      • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Kamati ya fedha, Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya Uchumi Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya UKIMWI (CMAC)
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba ya vikao vya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Maeneo ya uwekezaji
    • Bajeti
      • 2016/2017 Budget
    • TASAF
    • Mpango Mkakati
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • sheria
    • Fomu mbalimbali
    • Zabuni
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • video
    • Hotuba
    • Picha
    • Habari

PPRA YAWAPIGA MSASA WALIMU WAKUU, WATENDAJI KATA MAGU KUHUSU MATUMIZI MFUMO NeST

Posted on: May 27th, 2025

ZAIDI ya watumishi 300 ambao ni walimu wakuu, walimu wa ununuzi, watendaji wa kata na wa vijiji katika Halmashauri ya Wilaya ya Magu wamepewa mafunzo kuhusu usimamizi na ununuzi wa umma kielektroniki (NeST), ili waelewe namna ya kuomba zabuni, kusaini mikataba na kuitekeleza.

Mafunzo hayo yanayotolewa na Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA), yanafanyika katika ofisi za Halmashauri ya wilaya Magu mkoani Mwanza kwa siku tatu kuanzia Mei 26 hadi 28, 2025.

Mafunzo hayo pia yanahusisha wazabuni na maofisa ununuzi kutoka idara za ununuzi ya halmashauri ya Magu.

Akizungumza kwenye mafunzo hayo, Afisa Ununuzi Mwandamizi wa PPRA kanda ya Ziwa, Evaristo Mtilega, amesema kuwa licha ya mfumo huo kuanza kufanya kazi tangu 2023, sasa kinachoendelea ni kuuboresha na kuongeza moduli mpya zitakazoongeza ufanisi wa utekelezaji wa ununuzi wa umma nchini.

Akifungua mafunzo hayo, Mkuu wa Idara ya Manunuzi, Hilda Mwangamila amewataka wadau hao ununuzi kutumia mfumo wa NeST ipasavyo ili kusaidia kupata wazabuni wenye gharama zinazolingana na thamani ya fedha zinazolipwa.

Aidha, amewataka walimu hao na watendaji kuzingatia muongozo mpya wa ununuzi kwa sababu umeongeza uwazi.

"Mfumo huu wa kielektroniki umeundwa ili kuboresha uwazi, ushindani na usawa katika michakato ya manunuzi ya umma, hivyo tunaamini kwa mafunzo haya yatasaidia kutatua changamoto hususani kuharakisha michakato ya manunuzi ya vifaa vya ujenzi na upatikanaji wa mafundi kwani mfumo ni rafiki na kufanikisha miradi ya maendeleo kumalizika kwa wakati,” amesema na kuongeza;

“Ukiona umekosea usisite kuja ofisini kwetu kupata maelekezo kwa sababu ninyi ni sisi na sisi ni ninyi… milango ipo wazi, ninaamini waliopita kwenye mikono yangu wamepata maelekezo mazuri.

“Pia tumekubaliana wote kama kitengo kwamba jukumu letu la kwanza mpaka la tatu ni kuwahudumia ninyi vizuri ili documents zenu zikae vizuri. Kuna hoja za risiti nataka niwaase kuwa wazabuni sio ndugu zetu, mnapokuja kulipa hakikisha umeambatanisha na risiti kwani lengo sio kuwakomoa… ni kuhakikisha umeondokana na hoja za risiti. Kwa hiyo usimpe malipo kabla ya kukupa risiti. Hoja zinatesa, tukubaliane wote kwa pamoja kufuta hoja za manunuzi,” amesema Mwangamila.

Naye mmoja wa walimu walioshiriki mafunzo hayo, Hyahasisi Husein Msigala ambaye ni mwalimu wa ununuzi katika shule ya msingi Busekwa iliyopo kata ya Bujashi amesema mafunzo hayo yamewaongezea mbinu ya kusimama miradi ya maendeleo kwa uzalendo.

Amesema miongoni mwa mafunzo waliyofundishwa ni namna ya kufanya majadiliano kati ya mzabuni na taasisi za ununuzi ili kuweka vizuri makubaliano katika mkataba utakaokuja kusainiwa.

Matangazo

  • TANGAZO LA MAJINA YA WAANDISHI NA WAENDESHA VIFAA WALIOTEULIWA KATIKA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA AWAMU YA II April 28, 2025
  • TANGAZO LA UUZAJI WA VIWANJA HALMASHAURI YA WILAYA YA MAGU ENEO LA ILUNGU NA IGUDIJA TAREHE 02/12/2024 December 01, 2024
  • TANGAZO KWA UMMA November 18, 2022
  • FOMU ZA KUJIUNGA SHULE YA WASICHANA YA MKOA WA MWANZA MWANZA GIRLS SS 2023 December 16, 2022
  • Angalia zote

Habari mpya

  • PPRA YAWAPIGA MSASA WALIMU WAKUU, WATENDAJI KATA MAGU KUHUSU MATUMIZI MFUMO NeST

    May 27, 2025
  • Mchengerwa aagiza maofisa habari kukabidhiwa ofisi

    May 23, 2025
  • MAGU YAMSHUKURU RAIS SAMIA KWA KUENDELEA KUINUA KIUCHUMI KUNDI LA VIJANA

    May 21, 2025
  • MAGU YATENGA MILIONI 92 KUTENGENEZA MADAWATI 1300

    May 21, 2025
  • Angalia zote

Video

Serikali yatoa Matrekata 33 katika Halmashauri ya Wilaya ya Magu
More Videos

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Ugonjwa
  • Fomu ya Kusafiri nje ya Kituo cha kazi
  • Sheria ndogo za Halmashauri
  • Fomu ya Opras
  • Fomu Mpya ya Maombi ya Likizo kwa watumishi
  • Fomu ya Quotation ya likizo
  • Taratibu za mikutano na uendeshaji shughuli za Halmashauri
  • Mwongozo wa Uwekezaji Mkoa wa Mwanza
  • Utaratibu wa kutoa Leseni ya Biashara

Viunganishi Linganifu

  • Wakala ya Serikali Mtandao.
  • Wizara ya Afya
  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti kuu ya serikali
  • Ofisi ya Taifa ya takwimu Tanzania
  • tovuti ya Ikulu
  • Tovuti ya Mkoa wa Mwanza

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Magu. Haki zote zimehifadhiwa