• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
    • Malalamiko |
MAGU DISTRICT COUNCIL
MAGU DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Magu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Orodha ya viongozi Waliopita
      • Wenyeviti wa Halmashauri
      • Wakurugenzi
      • Wakuu Wa Wilaya
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Ardhi na Maliasili
      • Kilimo , umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Utumishi na utawala
      • Idara ya Mipango
      • Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Ujenzi
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Fedha
    • Vitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Ugavi
      • Kitengo cha Tehama
      • Internal Audit Unit
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kivutio cha Utalii
      • Bujora
    • Miundombinu ya Umwagiliaji
  • Huduma
    • Afya
    • Maji
    • Elimu
    • Kilimo
  • Madiwani
    • Baraza la Madiwani
      • Wajumbe wa Baraza la Madiwani
      • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Kamati ya fedha, Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya Uchumi Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya UKIMWI (CMAC)
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba ya vikao vya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Maeneo ya uwekezaji
    • Bajeti
      • 2016/2017 Budget
    • TASAF
    • Mpango Mkakati
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • sheria
    • Fomu mbalimbali
    • Zabuni
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • video
    • Hotuba
    • Picha
    • Habari

MCHENGERWA: JITOKEZENI KUGOMBEA NAFASI ZA UONGOZI WA SERIKALI ZA MITAA

Posted on: October 21st, 2024

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mohamed Mchengerwa amewataka wananchi wenye sifa za kugombea nafasi za uongozi wa Serikali za Mitaa, kujitokeza kuchukua na kurudisha fomu kuanzia tarehe 26 Oktoba hadi tarehe 1 Novemba, 2024 ili waweze kutimiza haki yao ya kikatiba ya kugombea katika uchaguzi utakaofanyika Novemba 27, 2024.

Waziri Mchengerwa ametoa wito huo kwa watanzania wenye sifa, wakati akitoa tathmini ya uandikishaji wa wapiga kura wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa mara baada ya kujiandikisha katika kituo cha Michikichini Kijiji cha Umwe Kaskazini Wilayani Rufiji.

“Zoezi la kuchukua na kurudisha fomu litafanyika kwa siku zote hizo kuanzia Oktoba 26 hadi Novemba 01, 2024 na kuongeza kuwa, muda wa kampeni utakapofika zifanyike kampeni za kistaarabu ambazo zitadumisha hali ya utulivu na Amani nchini,” Mchengerwa alisisitiza.

Waziri Mchengerwa amewashukuru wananchi wote, wanachama na wapenzi wa vyama vyote vya siasa kwa kuendelea kuonesha ukomavu wa kisiasa kwa kufanya siasa za kistaarabu, siasa za hoja na si za ugomvi mpaka zoezi la uandikishaji likifikia ukomo.

“Niwasihi tuendelee kufanya siasa za kistaarabu na ninawakemea vikali wanaotaka kuleta siasa za ugomvi ambazo zinaweza kuhatarisha amani na utulivu tulionao katika taifa,” Mchengerwa ameeleza.

Aidha, Mchengerwa amevisihi na kuvitaka vyombo vya dola viendelee kuhakikisha amani na utulivu unaendelea kuwepo katika kipindi chote cha mchakato wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ili wananchi waweze kushiriki kikamilifu Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

Sanjari na hilo, Waziri Mchengerwa amewasisitiza wasimamizi wa uchaguzi na wadau wote wa Uchaguzi wa Seriksali za Mitaa kuendelea kuzingatia Sheria na Kanuni za Uchaguzi, ili mchakato mzima wa uchaguzi uendeshwe kwa kuzingatia misingi ya Sheria na Kanuni zilizowekwa.

Matangazo

  • TANGAZO LA MAJINA YA WAANDISHI NA WAENDESHA VIFAA WALIOTEULIWA KATIKA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA AWAMU YA II April 28, 2025
  • TANGAZO LA UUZAJI WA VIWANJA HALMASHAURI YA WILAYA YA MAGU ENEO LA ILUNGU NA IGUDIJA TAREHE 02/12/2024 December 01, 2024
  • TANGAZO KWA UMMA November 18, 2022
  • FOMU ZA KUJIUNGA SHULE YA WASICHANA YA MKOA WA MWANZA MWANZA GIRLS SS 2023 December 16, 2022
  • Angalia zote

Habari mpya

  • WADAU WA SANAA MAGU WATAKIWA KUJISAJILI BASATA

    May 07, 2025
  • INEC YARIDHISHWA UBORESHAJI DAFTARI LA WAPIGA KURA MAGU

    May 03, 2025
  • DC Magu:Wazazi pelekeni watoto wapate chanjo ya polio

    April 30, 2025
  • WAANDISHI, WAENDESHA BVR 136 WALA KIAPO MAGU

    April 29, 2025
  • Angalia zote

Video

Serikali yatoa Matrekata 33 katika Halmashauri ya Wilaya ya Magu
More Videos

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Ugonjwa
  • Fomu ya Kusafiri nje ya Kituo cha kazi
  • Sheria ndogo za Halmashauri
  • Fomu ya Opras
  • Fomu Mpya ya Maombi ya Likizo kwa watumishi
  • Fomu ya Quotation ya likizo
  • Taratibu za mikutano na uendeshaji shughuli za Halmashauri
  • Mwongozo wa Uwekezaji Mkoa wa Mwanza
  • Utaratibu wa kutoa Leseni ya Biashara

Viunganishi Linganifu

  • Wakala ya Serikali Mtandao.
  • Wizara ya Afya
  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti kuu ya serikali
  • Ofisi ya Taifa ya takwimu Tanzania
  • tovuti ya Ikulu
  • Tovuti ya Mkoa wa Mwanza

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Magu. Haki zote zimehifadhiwa