• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
    • Malalamiko |
MAGU DISTRICT COUNCIL
MAGU DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Magu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Orodha ya viongozi Waliopita
      • Wenyeviti wa Halmashauri
      • Wakurugenzi
      • Wakuu Wa Wilaya
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Ardhi na Maliasili
      • Kilimo , umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Utumishi na utawala
      • Idara ya Mipango
      • Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Ujenzi
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Fedha
    • Vitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Ugavi
      • Kitengo cha Tehama
      • Internal Audit Unit
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kivutio cha Utalii
      • Bujora
    • Miundombinu ya Umwagiliaji
  • Huduma
    • Afya
    • Maji
    • Elimu
    • Kilimo
  • Madiwani
    • Baraza la Madiwani
      • Wajumbe wa Baraza la Madiwani
      • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Kamati ya fedha, Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya Uchumi Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya UKIMWI (CMAC)
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba ya vikao vya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Maeneo ya uwekezaji
    • Bajeti
      • 2016/2017 Budget
    • TASAF
    • Mpango Mkakati
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • sheria
    • Fomu mbalimbali
    • Zabuni
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • video
    • Hotuba
    • Picha
    • Habari

MAGU WASHIRIKI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU MWANZA

Posted on: October 6th, 2024

MKUU wa Wilaya ya Magu, Joshua Nassari leo tarehe 6 Oktoba, 2024 amewaongoza viongozi na watumishi wa halmashauri ya wilaya hiyo kuupokea Mwenge wa Uhuru ambao umetokea mkoani Geita na kupokewa katika Halmashauri ya Buchosa mkoani Mwanza.

Mbali na shamrashamra za kuupokea Mwenge huo zilizoanza mapema saa 11: 00 asubuhi, Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Said Mtanda ndiye aliyekabidhiwa Mwenge huo na Mkuu wa mkoa wa Geita, Martin Shigela.

Akizungumza kwenye mapokezi hayo yaliyofanyika kwenye kijiji cha Nyamadoke Halmashauri ya Buchosa wilayani, Sengerema, Mtanda amesema Mwenge wa Uhuru utakimbizwa katika wilaya 7 na Halmashauri 8 katika umbali wa zaidi ya kilometa 649.

Amesema Mwenge huo utatembelea, kukagua, kuweka mawe ya msingi na kuzindua miradi 58 ya maendeleo yenye thamani ya zaidi ya bilioni 98.

Ametaja miradi hiyo kuwa inahusu sekta za maji, elimu, afya, kilimo na miundombinu hasa ikizingatiwa mkoa huo wa Mwanza unachangia pato la Taifa kwa asilimia 7.2.

Naye Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa, Godfrey Mnzava amesema anatarajia kuona miradi hiyo katika mkoa wa Mwanza ikiwa kwenye ubora wa kuridhisha huku ile ambayo itawekwa mawe ya uzinduzi akitarajia kuwa itakamilika kwa wakati.

Tayari mkuu wa mkoa wa Mwanza amemkabidhi Mwenge huo wa Uhuru kwa Mkuu wa Wilaya ya Sengerema, Seni Ngaga kwa ajili ya kukimbiza kwenye halmashauri ya Buchosa leo tarehe 6 Oktoba 2024.

Mbio za Mwenge mwaka huu zinaongozwa na kauli mbiu isemayo; "Tunza mazingira, "Shiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa Ujenzi wa Taifa Endelevu".

Matangazo

  • TANGAZO LA MAJINA YA WAANDISHI NA WAENDESHA VIFAA WALIOTEULIWA KATIKA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA AWAMU YA II April 28, 2025
  • TANGAZO LA UUZAJI WA VIWANJA HALMASHAURI YA WILAYA YA MAGU ENEO LA ILUNGU NA IGUDIJA TAREHE 02/12/2024 December 01, 2024
  • TANGAZO KWA UMMA November 18, 2022
  • FOMU ZA KUJIUNGA SHULE YA WASICHANA YA MKOA WA MWANZA MWANZA GIRLS SS 2023 December 16, 2022
  • Angalia zote

Habari mpya

  • WADAU WA SANAA MAGU WATAKIWA KUJISAJILI BASATA

    May 07, 2025
  • INEC YARIDHISHWA UBORESHAJI DAFTARI LA WAPIGA KURA MAGU

    May 03, 2025
  • DC Magu:Wazazi pelekeni watoto wapate chanjo ya polio

    April 30, 2025
  • WAANDISHI, WAENDESHA BVR 136 WALA KIAPO MAGU

    April 29, 2025
  • Angalia zote

Video

Serikali yatoa Matrekata 33 katika Halmashauri ya Wilaya ya Magu
More Videos

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Ugonjwa
  • Fomu ya Kusafiri nje ya Kituo cha kazi
  • Sheria ndogo za Halmashauri
  • Fomu ya Opras
  • Fomu Mpya ya Maombi ya Likizo kwa watumishi
  • Fomu ya Quotation ya likizo
  • Taratibu za mikutano na uendeshaji shughuli za Halmashauri
  • Mwongozo wa Uwekezaji Mkoa wa Mwanza
  • Utaratibu wa kutoa Leseni ya Biashara

Viunganishi Linganifu

  • Wakala ya Serikali Mtandao.
  • Wizara ya Afya
  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti kuu ya serikali
  • Ofisi ya Taifa ya takwimu Tanzania
  • tovuti ya Ikulu
  • Tovuti ya Mkoa wa Mwanza

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Magu. Haki zote zimehifadhiwa