Mkuu wa Wilaya ya Magu Mh.Joshua Nassari leo Jumatatu Julai 1 , 2024 ameongoza kikao maalum cha kamati ya ushauri ya Wilaya DCC kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano ya Halmashauri.
Kikao hicho kilihudhuriwa na wajumbe mbalimbali akiwemo Waziri wa Ulinzi na jeshi la kujenga Taifa Mheshimiwa Dkt. (Mb) Stregomena Taxi , Watendaji wa Kata, Wakuu wa idara na vyama rafiki kilijadili mambo mbalimbali ikiwemo mapendekezo ya kugawa jimbo la Magu, kupokea taarifa ya miradi ya maendeleo , taarifa ya mapato, matumizi ya sheria ndogo za mazingira na kupokea taarifa za taasisi.
Akizungumza wakati wa kikao hicho DC Nassari ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Magu kwa kufikia asilimia 97% ya kukusanya mapato kwa mwaka wa fedha 2023-2024 huku akitoa wito kuendelea kushirikiana katika kukusanya mapato ili kuendelea kutekeleza miradi ya maendeleo.
Aidha amesema mchakato wa kupima viwanja katika eneo la Igekemaja kata ya Kisesa utaendelea ili kupanga mji na kurahisisha upatikanaji wa huduma muhimu za kijamii katika maeneo yaliyopimwa.
Kwa upande wake Waziri wa ulinzi na jeshi la kujenga Taifa Mh. Stargomena Taxi ameshauri elimu zaidi itolewe ili kuwajengea uelewa wananchi kuhusu kuanza kwa utekelezaji wa sheria ndogo za mazingira .
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Magu. Haki zote zimehifadhiwa