Mkuu wa Wilaya ya Magu Mh. Joshua Nassari ameongoza kikao cha kamati ya sherehe ya mapokezi ya mwenge wa uhuru wa uhuru Wilayani Magu ambao unatarajiwa kuwasili Wilayani hapa Oktoba 10, 2024.
Akizungumza wakati wa kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri DC Nassari amezielekeza idara zenye miradi itakayopitiwa ma mwenge wa uhuru kuendelea na maandalizi ili kuweka miradi katika hali inayotakiwa .
Mwenge wa uhuru 2024 unakimbizwa ukiwa na kauli mbiu ya Tunza Mazingira na shiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa ujenzi wa Taifa endelevu".
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Magu. Haki zote zimehifadhiwa