Aliyekua Mkuu wa Wilaya ya Magu Rachel Kassanda, amekabidhi rasmi ofisi kwa Mkuu wa Wilaya ya Magu Mh. Joshua Nassari leo Jumatano Machi 13, 2024 mara baada ya uhamisho uliofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Dkt Samia Suluhu Hassan Machi 9, 2024 ambapo alimuhamisha Mh Nassari kutoka Wilaya ya Monduli na kua Mkuu wa Wilaya ya Magu.
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo DC Nassari amemshukuru Rais Dkt Samia kwa kuendelea kumuamini na kumhamisha kuja kuwatumikia wananchi wa Magu huku akiomba ushirikiano kwa kamati ya ulinzi na usalama, wakuu wa idara , taasisi na watumishi wote wa Wilaya ya Magu katika kutekeleza majukumu mbalimbali ya kuwahudumia wananchi.
Aidha Dc Nassari amesema kua hajaja Wilayani Magu kubadilisha utaratibu uliopo bali ni kuendeleza mazuri yaliyokuwepo ili kuendelea kuwatumikia wananchi wa Magu.
Kwa upande wake Rachel Kassanda amewashukuru watumishi na wafanyakazi wa Wilaya ya Magu kwa ushirikiano waliomuonyesha katika kipindi chote cha uongozi wake.
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Magu. Haki zote zimehifadhiwa