Tangazo la Usafi wa Mazingira Mwisho wa Mwezi
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Magu, anawatangazia watumishi wote wa Serikali kuwa kila jumamosi ya Mwisho wa mwezi ni siku ya usafi. Hivyo watumishi wote mnatakiwa kufika makao makuu ya wilaya Jumamosi ya tarehe 25.02.2017 ambayo ni Jumamosi ya mwisho wa mwezi Februari mkiwa na vifaa vya usafi tayari kwa kufanya usafi kuanzia saa 1:30 asubuhi hadi saa 3:30 asubuhi.
Baada ya shughuli za usafi kumalizika Viongozi wa wilaya wataongea na watumishi wote walioshiriki katika shughuli hiyo ya usafi. Mtumishi ambaye hatafika bila taarifa atachukuliwa hatua za kinidhamu.
N:B: Usafi ni ustaarabu, tujenge tabia ya kuwa wasafi siku zote.
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Magu. Haki zote zimehifadhiwa